Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
akizungumza katika kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti wa Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba ya wilaya pamoja na Wasajili Wasaidizi mkoani Tanga.
Sehemu
ya washiriki wa kikao kazi na mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba ya Wilaya pamoja na Wasajili wasaidizi wakifuatilia
hotuba ya Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete wakati wa ufunguzi wa
kikoa hicho
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi
akizungumza kwenye kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti wa Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba ya wilaya pamoja na Wasajili Wasaidizi mkoani Tanga
Msajili
wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo akizungumza
katika kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na
Nyumba ya wilaya pamoja na Wasajili Wasaidizi mkoani Tanga
Mkuu
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza katika kikao kazi na
mafunzo cha wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya pamoja na
Wasajili Wasaidizi mkoani Tanga
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
akisalimiana na mmoja wa wenyeviti wa Baraza laAardhi na Nyumba la
Wilaya wakati wa kikao kazi na maafunzo kinachoendelea mkoani Tanga.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na wenyeviti wa Mabaraza ya ardhi na nyumba ya
wilaya wakati wa kikao kazi na mafunzo kinachofanyika mkoani Tanga
(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
………………………………………………………………..
Na Munir Shemweta, WANMM TANGA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
amewataka Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kuwa
waadilifu sambamba na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kutenda haki
wakati wa kutoa maamuzi ya mashauri yanayohusu migogoro ya ardhi.
Aidha, alizitaka Mamlaka za Nidhamu kuwachukulia hatua za kinidhamu
watumishi wote wasiotimiza wajibu wao au wanaoidhalilisha serikali kwa
kuendesha vitendo vya rushwa.
Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na
nyumba ya wilaya nchini pamoja na Wasajili Wasaidizi wanakutana mkoani
Tanga kwenye kikao kazi na mafunzo cha siku nne kujadiliana namna bora
ya kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma bora kwa wananchi kuhusiana
mashauri ya ardhi.
‘’Daima tukumbuke ili mabaraza ya ardhi
yaweze kuheshimika ni wajibu wenu wenyeviti wa mabaraza kama watumishi
wa umma kufanya kilicho sahihi yaani kuzingatia weledi, kuwa waadilifu
na kuwajibika. Tukumbuke kuwa sisi ni watumishi wa umma ni waajiriwa wa
wananchi‘’ alisema Ridhiwani
Akizungumza kwenye kikao kazi na
Mafunzo mkoani Tanga tarehe 5 April 2022 Naibu Waziri wa Ardhi alisema,
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya kama vyombo vya kutoa haki yana
wajibu wa kuhakikisha yanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuondoa
malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa maadili katika kushughulikia migogoro
ya ardhi.
‘’Haki na wajibu ni sawa na chanda na pete katika
uwajibikaji wa daraja la juu. Mtekelezaji wa utoaji au usimamizi wa
halki bila kuwa muadilifu ni mtihani mkubwa’’ alisema Ridhiwani.
Alieleza
kuwa, maadili ni kitu muhimu cha kuzingatia katika utendaji kazi hasa
kipindi hiki ambacho serikali ya wamu ya sita inafanya juhudi mbalimbali
kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanazingatia maadili yanayosimamaia
utumishi wa umma.
‘’Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika matamshi
yake, mbalimbali ameonesha wazi nia yake ya kuurejesha utumishi wa umma
kuwa utumishi uliotukuka na unaozingatia taratibu za utendaji na
maadili yanayoongoza utumishi wa umma’’ alisema Ridhiwani.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt Allan Kijazi alisema, Wizara yake itaanza kuweka mfumo wa
ufuatiliaji utendaji kazi wa wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kwa lengo la
kuboresha utendaji kazi.
‘’Katika mfumo huo wa ufuatiliaji wale
wenyeviti ambao utendaji wao utaridhisha tutakuwa pamoja na wale
wasiotaka kubadilika itabidi watupishe na tutafute watendaji au
wenyeviti walio tayari kutekeleza majukumu na wako tayari kutenda haki
na watanzania wote bila kubagua lakini kikubwa zaidi kuwa tayari
kubadilisha taswira ya wizara ya kiutendaji kutoka wizara ya malalamiko
na kuwa wizara yenye kupewa sifa nzuri za utendaji’’ alisema Dkt Kijazi.
Naye Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini
Stella Tullo alielezea mafunzo waliyoyapata wenyeviti wa Mabaraza ya
ardhi nchini alisema kuwa, yatawajengea uwezo na anaamini mara baada ya
kujifunza watakaporudi kwenye vituo vyao vya kazi watakuwa na nafasi
nzuri ya kusikiliza mashauri ya ardhi sambamba na kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, April 6, 2022
RIDHIWANI AWATAKA WENYEVITI MABARAZA YA ARDHI KUJIEPUSHA NA RUSHWA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment