RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni
miongoni mwa Watanzania waliopewa Tuzo ya Heshima kupitia Tuzo za Muziki
Tanzania 2021.
Mheshimiwa
Rais Samia amepewa heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa
alioutoa katika sanaa na burudani ambapo ametenga zaidi ya shilingi
Bilioni 1.5 kufanikisha heshima hiyo ambayo ilikosekana kwa miaka zaidi
ya saba iliyopita.
Tuzo
hizo zilizoratibiwa na Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa chini
ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zimetolewa usiku wa kuamkia leo
Aprili 3, 2022 katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.
BASATA
ni taasisi ya umma iliyoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984
kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019.
Historia
inaonesha kuwa, sheria ya kuunda upya baraza hilo ilifanywa kwa
kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza
la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili
lisimamie maendeleo ya sanaa nchini
Aidha,
tuzo hiyo ya heshima imeenda kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,
Jenerali Venance Mabeyo,aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba, Fatima binti Baraka
maarufu kama Bibi Kidude,staa wa muziki ndani na nje ya Tanzania ambaye
pia ni Mtendaji Mkuu wa WCB,Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz).
Tuzo nyingine
Malikia
aliyetwaa tuzo katika video ya mwaka 2021 ni Feven Reuben (Fevushka),
Mfalme aliyetwaa tuzo katika video ya mwaka 2021 ni Selemani Masenga.
Mnenguaji bora wa kike mwaka 2021 ni Baby Drama huku kwa upande wa mnenguaji bora wa kiume akitoka Kukaye Moto Culture Centre.
Pia
mwimbaji bora wa kike nyimbo za asili mwaka 2021 ni Shoninda Kilasi,
mwanamuziki bora wa kiume wa muziki wa asili 2021 ni Msafiri Zaosa na
wimbo bora wa asili 2021 ni Asili Yetu ya Sholo Mwamba.
Msanii
bora wa kike kwa upande wa muziki wa mwambao (Taarab) 2021 ni Khadija
Yusuf huku nafasi ya msanii bora wa kiume katika muziki huo akiwa ni
Mzee Yusuf ambapo wimbo bora wa Taarab 2021 ni Usinifokee Jahazi Modern
Taarab.
Kwa
upande wa mwanamuziki bora wa Reggae/dancehall 2021 ni Badest 47 huku
wimbo bora wa Reggae/Dancehall ukiwa ni Unaota wa Badest 47.
Aidha,
tuzo ya mtumbuizaji bora wa kike wa mwaka 2021 ameshinda Saraphina
Michael ambapo tuzo hiyo ilikuwa na washindani kama Shilole, Nandy na
Maua Sama.
Nafasi
ya tuzo ya mtumbuizaji bora wa kiume 2021 kwenye tuzo hizo imechukuliwa
na staa wa muziki ndani na nje ya Tanzania,Rajab Abdul Kahali
(Harmonize) ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Konde Music Worldwide baada
ya kuwaangusha Sholo Mwamba, Alikiba,Whozu na Dulla Makabila.
Wakati
huo huo, msanii bora wa kiume wa singeli wa mwaka 2021 ni Sholo Mwamba,
wimbo bora wa mwaka wa singeli ni Alowee na Sholo Mwamba, hivyo
ukijumlisha na tuzo ile ya wimbo wa asili wa mwaka huu ambao ulikuwa ni
Asili Yetu atakuwa kazoa tuzo tatu.
Mshindi
wa Tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana 2021 ni Loyalty ya Darassa
akiwashirikisha Marioo na Nandy ambapo wameiangusha Ndombolo ya Alikiba,
Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour, Shikilia ya Profesa J, Unaua vibe ya
Rapcha na Lala ya Jux.
Naye
mwimbaji Nandy ameshinda Tuzo ya Chaguo la Watu kwenye Majukwaa ya
kidigitali mtandaoni kama mwimbaji bora wa kike 2021.Mtunzi bora wa
mashairi wa mwaka 2021 ameshinda Profesa Jay kupitia Utaniambia Nini
baada ya kuwaangusha Alikiba akiwa na Utu, Mi amor ya Marioo, Lisa ya
Rapcha na Loyalty ya Darassa.
Wakati
huo huo, tuzo ya mtunzi bora wa melody wa mwaka 2021 imeenda kwa
Alikiba huku albamu bora ya mwaka 2021 ikiwa ni Only One King ya
Alikiba.
Tuzo
ya mwanamuziki bora wa kiume chaguo la watu kwenye majukwaa ya
kidigitali ni Alikiba huku akichukua tena tuzo ya mwanamuziki bora
Afrika Mashariki wa mwaka 2021
Kwa
upande wa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa Hiphop 2021 imeenda
kwa Zombie, huku Mr.T Touch akishinda tuzo ya mtayarishaji bora wa
Bongofleva kwa mwaka 2021.
Wakati
huo huo, mwimbaji wa Bongo fleva Saraphina Michael ametwaa tuzo
nyingine ya msanii bora chipukizi upande wa kike kwa mwaka 2021. Huku
Rapcha akitwaa Tuzo ya Msanii bora chipukizi wa kiume kwa mwaka 2021.
Tuzo
ya Mwanamuziki Bora wa kiume wa Bongofleva mwaka 2021 imeenda kwa
Marioo, huku Young Lunya akishinda tuzo mbili ikiwemo ya msanii bora wa
Hiphop na wimbo bora wa Hiphop wa Mbuzi. Naye Chemical ameshinda Tuzo ya
Msanii bora wa kike wa Hiphop 2021.
Mhariri DIRAMAKINI ataendelea kuongezea maudhui na kuboresha zaidi habari hii, endelea kufuatilia
No comments:
Post a Comment