Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.
Augustine Mwarija amezindua rasmi Jarida la Mahakama ya Rufani (Court
of Appeal Journal) huku akisisitiza Wananchi kusoma Jarida hilo ambalo
linapatikana pia kupitia tovuti ya Mahakama ya www.judiciary.go.tz.
Akizungumza
kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma jana
tarehe 05 Aprili, 2022 katika Ukumbi wa ‘Mount Meru’ jijini Arusha, mara
baada ya kulizindua Jarida hilo, Jaji Mwarija amesema kuwa lengo la
kuwa na Jarida hilo ni kuujuza umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu
Mahakama ya Rufani na kuondoa baadhi ya maswali ambayo yamekuwa
yakiulizwa na wananchi.
“Kumekuwa na maswali mengi ya jinsi
Mahakama ya Rufani inavyofanya kazi, mathalani wengi wamekuwa
wakijiuliza katika jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufani ni nani
anayeandika hukumu na maswali mengineyo, hivyo ni vyema kulisoma Jarida
hili ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu Mahakama ya Rufani (T) ikiwa
ni pamoja na kufahamu historia ya Mahakama ya Rufani na kadhalika,”
amesema Jaji Mwarija.
Jaji Mwarija ameongeza kuwa Jarida hilo
lililopo kwenye lugha ya Kiingereza linaeleza utendaji wa Mahakama ya
Rufani na vilevile linaonyesha ufanisi pamoja na historia ya Mahakama
hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka.
“Wengi pia watajiuliza
kwanini Jarida hili lipo kwenye Lugha ya Kiingereza, tumefanya hivi kwa
kuanzia lakini mpango tulionao katika toleo zijazo ni kutumia Lugha zote
mbili katika Jarida hili ili kuwawezesha Wadau wote waweze kuelewa
kilichoandikwa,” amesema Jaji huyo.
Kwa upande wake Msajili wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina amesema kuwa wazo la kuanzisha
Jarida hilo la mwaka 2021 lilianzia kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Prof. Ibrahim Hamis Juma.
“Wazo la kuanzisha Jarida hili
lilianzia kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma na
tumelitekeleza, na Jarida hili ni la mwaka 2021 lina taarifa mbalimbali
ikiwa ni pamoja na takwimu mbalimbali zinazoonyesha utendaji wa
Mahakama, historia ya kuanzishwa kwake, orodha ya Majaji wa Mahakama
hiyo na mengineyo,” amesema Mhe. Mhina.
Aidha, Msajili huyo ameishukuru Timu nzima iliyowezesha kufanikisha upatikanaji wa Jarida hilo na kuomba ushirikiano zaidi.
Jarida
hilo limezinduliwa leo ikiwa ni siku ya pili ya Kikao kazi cha Mapitio
ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa mwaka 2020/2021-2024/2025
kinachokwenda sambamba na kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za
Mahakama kinachoendelea kufanyika jijini Arusha.
Mahakama ya
Tanzania inaendelea kuuhabarisha umma kwa njia mbalimbali mojawapo ikiwa
ni kupitia Majarida yake ya ‘Haki Bulletin’ linalotolewa mara nne kwa
mwaka pamoja na Jarida hilo la Mahakama ya Rufani lililozinduliwa ambalo
litakuwa likitolewa mara moja kwa mwaka.
Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Augustine Mwarija (kushoto)
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jarida la Mahakama ya Rufani
(T). Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana tarehe 05 Aprili, 2022 katika
Ukumbi wa 'Mount Meru' jijini Arusha ambapo kinafanyika Kikao kazi cha
Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa mwaka
2020/2021-2024/2025 sambamba na kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za
Mahakama. Wanaoshuhudia, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, Mhe. Joachim Tiganga, wa pili kulia ni
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma na wa kwanza
kulia ni Mhe. Happiness Ndesamburo, Naibu Msajili Mwandamizi-Mahakama ya
Rufani (T).
Nyuso
za furaha mara baada ya uzinduzi wa Jarida la Mahakama ya Rufani (T)
uliofanyika jana tarehe 05 Aprili, 2022 katika Ukumbi wa 'Mount Meru'
jijini Arusha.
Msajili
wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina akizungumza wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi wa Jarida la Mahakama ya Rufani (T).
Sehemu
ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu na
Washiriki wengineo walioshuhudia uzinduzi wa Jarida la Mahakama ya
Rufani (Court of Appeal Journal).
Jaji
wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Augustine Mwarija (katikati) na wenzake
wakiwa wameshika nakala za Jarida la Mahakama ya Rufani alilozindua. Wa
tatu kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Mustapher Siyani, wa tatu kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha, Mhe. Joachim Tiganga, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, wa pili kulia ni
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, wa kwanza
kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina na wa kwanza
kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.
Happiness Ndesamburo.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, April 6, 2022
JARIDA LA MAHAKAMA YA RUFANI LAZINDULIWA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment