Waziri
Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk Jilly Maleko (wa tatu
kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa pili
kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu
kushoto), Mjumbe wa Bodi Benki ya CRDB Burundi, Kahumbaya Bashige
(wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fred
Siwale (wa kwanza kushoto), na Menard Bucumi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB Burundi.
Benki
ya CRDB inaonekana kuwa daraja muhimu la kukuza biashara na mahusiano
ukanda wa katika Afrika Mashariki, hasa miongoni mwa nchi za Tanzania,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Burundi.
Benki
hiyo kwa sasa inatoa huduma katika nchi ya Burundi na inaelezwa kuwa
katika robo ya tatu yam itazindua huduma zake kupitia kampuni tanzu huko
Lubumbashi, jiji la pili kwa ukubwa baada ya Kinshasa, nchini DRC.
Kuanzishwa
kwa kampuni tanzu hiyo kunaendana vyema na hatua za hivi karibuni
ambapo nchi ya DRC imekubaliwa ombi lake la kuwa mwanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kufanya jumla ya nchi saba wanachama
katika ukanda huu.
Waziri
Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni, alisema amefurahishwa kusikia
kwamba Benki ya CRDB inafungua kampuni yake tanzu nchini DRC
itakayokuwa na makao yake makuu mjini Lubumbashi na kutaka huduma hizo
kusogezwa karibu na mpaka wa Burundi na DRC pia.
"Ninaiomba
benki kufungua matawi karibu na mipaka ya Burundi na DRC, katika miji
ya Uvira na Bukavu ili kuimarisha biashara," Bunyoni alisema hayo wakati
alipotembelewa na ujumbe wa Benki ya CRDB ofisini kwake mwishoni mwa
juma lililopita kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inayoipa benki hiyo.
Ujumbe
huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt
Ally Lay na Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela, ambao waliambata Balozi wa Tanzania nchini Burundi,
Dkt Jilly Mareko.
Madhumuni
yalikuwa kwa wajumbe wa Kikundi cha Benki ya CRDB kufahamu msaada ambao
benki hiyo inapata kutoka kwa serikali ya Burundi tangu wakati
mkopeshaji alipofungua kampuni yake tanzu nchini Burundi mwaka 2012.
Katika
mazungumzo yaliyofanyika, Benki hiyo ilimhakikishia Bunyoni kuendelea
kushirikiana na serikali zote mbili za Burundi na Tanzania kufadhili
miradi ya pamoja inayofanywa na nchi hizo mbili hususan mradi wa reli ya
kisasa (SGR) na miradi mingineyo.
Waziri
Mkuu huyo aliishukuru Benki ya CRDB kwa kusaidia kukuza uchumi wa
Burundi kupitia uwezeshaji mkubwa inaoufanya nchini humo kwa kutoa
mikopo inayogusa makundi mbalimbali ya wateja kuanzia kupitia watu
binafsi, makampuni na hata serikali.
"Niwahakikishie
kuwa serikali yetu inaunga mkono jitihada mnazozifanya katika kuinua
uchumi wa Taifa letu la Burundi, na tupo tayari kushirikiana nanyi
katika utekelezaji miradi mikubwa kwani baadhi yao inahusisha hata nchi
zetu mbili za Tanzania na DRC," Bunyoni alisema.
Aliukumbusha
ujumbe wa benki hiyo kuwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanzisha huduma za
kibenki kupitia simu za mkononi nchini humo “SimBanking”, nakubainisha
kuwa huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa nchini humo na kuwa kichocheo
kikubwa katika kuongeza ujumuishi wa kifedha.
Pia
aliishukuru Benki ya CRDB kwa uwezo wake wa kukusanya fedha kwenye
masoko ya kimataifa bila masharti magumu kama ambavyo imekuwa ikifanywa
na baadhi ya wakopeshaji kutoka nje ya Afrika.
"Pia
ni muhimu kutambua kwamba benki hii kupitia programu yake ya mageuzi ya
kidijitali imekuwa ikisaidia kurahisha miamala ya kibiashara ya kati ya
Burundi na Tanzania kwa kuweka mifumo na miundo mbinu inayowezesha
miamala ya kifedha kufanyika kwa urahisi ikiwamo malipo ya bandari na
kodi mbalimbali zinazotozwa na serikali,” alioongezea.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Laay,
alimweleza Waziri Mkuu huyo kuwa benki hiyo imewekeza zaidi katika
mifumo ya kidijitali ili kuwawezesha wateja kuokoa muda na hata kupanua
huduma za benki katika maeneo ambayo hayajafikiwa.
"Hii itasaidia Burundi katika utekelezaji wa ajenda yake ya kuongeza ujumuishi wa kifedha," Dkt Laay alisema na kuongeza:
"Ni
katika muktadha huo benki sasa inasambaza huduma za CRDB Wakala
wajulikanao kama ‘Turihose’ nchini humo, pamoja na kuhamasisha matumizi
ya huduma za SimBanking, na huduma ya kibenki kupitia mtandao ‘Internet
banking’ kwa wateja wake.”
Sambamba
na miaka 10 ya Programu ya Maendeleo ya Taifa la Burundi, Mwenyekiti
huyo alisema, benki hiyo inatarajia kuelekeza nguvu zake katika
maendeleo ya sekta za kiuchumi kama vile kilimo, viwanda, miundombinu na
makazi, na utalii ambazo ni muhimu katika kukuza ajira kwa vijana na
kutengeza fedha za kigeni nchini humo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB alimweleza Waziri Mkuu Bunyoni
kuwa kwa sasa benki hiyo inashika nafasi ya tatu kwa utoaji wa mikopo
nchini Burundi baada ya miaka 10 ya kufanya kazi na asilimia 20 ya
mikopo yake imetolewa katika sekta ya ili kusaidia Warundi wengi.
"Katika
kipindi cha miaka kumi iliyopita, benki imeendelea kusaidia uchumi wa
Burundi kwa kutoa bidhaa na huduma bunifu kwa makampuni, watu binafsi na
taasisi wateja kupitia bidhaa za kuweka kuweka amana na mikopo,"
Nsekela alisema.
Hivi
Karibuni ujumbe wajumbe wa viongozi wa Chemba za Biashara za nchi za
Burundi, Misri, Zambia, Botswana, Rwanda, Ethiopia na Uganda ukiongozwa
na Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR
walitembelea makao makuu ya Benki ya CRDB na kupongeza mkakati wa benki
hiyo wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Benki
hiyo - ambayo imekuwa nchini Burundi tangu 2011 ina jumla ya matawi
manne, matatu Bujumbura na moja katika mji wa Ngozi, mwaka huu Benki ya
CRDB inatarajia kufungua tawi la tano katika Wilaya ya Gitega.
Akielezea
matokeo ya kifedha ya kampuni tanzu ya Burundi, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB Burundi, Fred Siwale amesema mwaka jana walipata faida ya
Shilingi bilioni 12.8 ikiwa niongezeko la asilimia 14 kulinganisha na
faida ya Shilingi bilioni 11.1 iliyopatikana mwaka 2020.
Benki
hiyo pia ilipata matokeo mazuri katika viashiria vingine vya utendaji;
Jumla ya Risilimali imeongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 551.1
kutoka Shilingi bilioni 350 iliyorekodiwa mwaka 2020, wakati amana za
wateja ziliongeka kwa asilimia 66 kufikia Shilingi bilioni 329.4
kulinganisha na Shilingi bilioni 198.6 iliyorekodiwa mwaka 2020.
Mikopo
iliongezeka kwa asilimia 62 kutoka Shilingi bilioni 225 mwaka 2020 hadi
Shilingi bilioni 598. Siwale alisema Benki hiyo imekuwa mlipakodi
mkubwa kwa serikali ya Burundi pamoja na kutengeneza ajira kwa Warundi.
No comments:
Post a Comment