MGANGA MKUU wa Serikali Dkt.
Aifello Sichalwe amewaelekeza viongozi wa jadi/mila nchini kuhakikisha
wanapambana na tatizo la vifo vya Wajawazito ambalo kwa kiasi kikubwa
linatokana na kuchelewa kwenda kliniki, mjamzito kutojifungulia katika
vituo vya kutolea huduma au kuchelewa kufika katika vituo hivyo.
Ameyasema
hayo alipofanya ziara ya kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya magonjwa
mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa kwa
jamii, shughuli iliyoambatana na zoezi la kumsimika kiongozi
(Olaigwanani) wa familia ya Napaya ambae pia ni Diwani wa kata ya
Ngabobo Mkoani Arusha Bw. Gabriel Kinwaa Mollel.
"Tunataka
mtusaidie sana katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kutumia
miundombinu/uwekezaji ambao Serikali imeufanya kwa kuhakikisha
wajawazito wanakwenda kliniki mapema lakini pia waweze kujifungulia
katika vituo vya kutolea huduma, hatutaki kuona mama anajifungulia
nyumbani halafu akafariki." Amesema.
Moja kati ya vipaumbele vya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Ally Mwalimu ni kuhakikisha suala la huduma
bora za mama na mtoto zinaboreshwa ili kuondoa vifo vinavyotokana na
uzazi vinavyoweza kuzuilika. Amesisitiza Dkt. Sichalwe.
Sambamba
na hilo, Dkt. Sichalwe amewataka viongozi kuhakikisha wanahamasisha
wananchi kujenga na kutumia vyoo ipasavyo ili kuepuka magonjwa ya
mlipuko hasa kipindupindu na magonjwa mengine ya matumbo yanayoweza
kuzuilika na kuipunguzia Serikali gharama za matibabu.
Pia, Dkt.
Sichalwe amewaomba Olaigwanani kuendelea kuhamasisha na kusisitiza
jamii zao juu ya umuhimu wa kupata Lishe bora, hususan kwa wamama
wajawazito na Watoto ili kujenga Taifa la watu wenye afya bora na uwezo
wa kufikiri katika kuleta Mapinduzi ya kimaendeleo katika ngazi ya jamii
mpaka Taifa.
Mbali na hayo, amesema Serikali imetimiza wajibu
wake wa kuleta maendeleo kwa Wananchi wake kwa kuboresha miundombinu ya
afya, elimu, barabara, umeme na maji ambayo kwa kiasi kikubwa inachochea
ukuaji wa shughuli za uchumi na kuwataka kuendelea kuitunza miundombinu
hiyo ili iendelee kuleta tija katika maeneo yao.
Nae, Diwani wa
kata ya Ngabobo na kiongozi wa familia ya Napaya Bw. Gabriel Kinwaa
Mollel amemshukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada za
kuboresha huduma kwa wananchi ikiwemo elimu ya kujikinga dhidi ya
ugonjwa mbalimbali na elimu ya huduma za mama na mtoto.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Sunday, April 3, 2022
HATUTAKI KUONA MJAMZITO ANAFIA NYUMBANI - DKT. SICHALWE.
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment