MFALME wa Muziki wa Bongofleva
Ali Saleh Kiba maarufu kama Alikiba ameng'ara kwenye Tuzo za Muziki
nchini zilizofanyika usiku wa kuamkia April 2 mwaka huu katika ukumbi wa
Mikutano cha Kimataifa (JNICC) jijini Dar es salaam.
Alikiba ameondoka na Tuzo Tano kupitia Album yake "Only 1 king" aliyoiachia mwishoni mwa mwaka 2021.
Alikiba
,ameshinda katika kipengele Cha Album bora, Msanii Bora wakiume wa
Mwaka,Mtunzi Bora wa Mashairi, video Bora ya mwaka, , Mwanamuziki bora
chaguo la watu.
Hata hivyo Alikiba hakuweza kuhudhuria katika
kilele cha tuzo hizo badala yake wawakilishi wake waliweza kuzipokea
tuzo na kuwashukuru watanzania Kwa kumpigia kura nyingi za kishindo.
Wawakilishi kutoka kundi la "Kings Music" wakipokea tuzo ya Msanii wa Muziki nchini Alikiba mara baada ya kushinda katika tuzo za Muziki zilizofanyika usiku wa April 2 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa JNICC Jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment