Waziri wa Afya Nassor Ahmed
Mazrui amesema Wizara yake inakusudia kuimarisha maabara na kuwapatia
mafunzo wafanyakazi wa sekta ya afya ili waweze kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Akizungumza na Ugeni kutoka Shirika la Misaada
Marekani ambao wanawakilisha OGAC na CDC huko ofisini kwake Mnazi Mmoja
amesema kupitia Shirika hilo watakuwa mstari wa mbele katika kupambana
na maambukizi ya UKIMWI.
Amesema wafanyakazi watapatiwa mafunzo
ya kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti ili kuongeza kiwango cha utoaji
huduma na kuimarisha sekta ya afya nchini.
“Katika kuwajenga
katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ni kuwajengea uwezo
wafanyakazi wa kufanya utafiti ambao utasaidia katika kutoa huduma bora
kwa jamii”, alisema Waziri Mazrui.
Ameeleza kuwa kupitia Shirika
hilo wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na UKIMWI nchini, hivyo
ameomba kuwepo na ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza janga hilo.
"Ni
kweli hivi sasa tuna waathirika wa UKIMWI 7600, waathirika 400 kwa
mwaka 2020 hadi 2021 hichi si kiwango kidogo katika Nchi yetu", amesema
Waziri Mazrui.
Waziri Mazrui amesisitiza jamii kuongeza juhudi
ya kutoa ushauri kwa walioathirika wasiwaambukize wengine, kuwapatia
matibabu kwa wale walioathirika ili waendelee kuishi vizuri.
Hata
hivyo Waziri Mazrui amesema wapo katika ujenzi wa hospital 10 za Wilaya
na moja ya Mkoa ambazo zina malengo ya kutoa huduma bora za afya kwa
jamii na jukumu kuu la sekta ya Afya ni kuimarisha afya za wananchi.
Amefahamisha
kuwa katika kupambana na maradhi ya kuambikiza Mke wa Rais Mama Maryam
Mwinyi yupo mstari wa mbele katika kupambana na kupinga maambukizi ya
UKIMWI nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ujumbe huo Michelle
Chevalier amesema lengo la Shirika hilo ni kuweka mashirikiano ya
karibu na sekta ya Afya katika mapambano ya kujikinga na maradhi ya
UKIMWI, viashiria vya maradhi hayo pamoja na kuwapatia huduma
waathirika.
Vile vile ameahidi kuweka mashirikiano katika suala
zima la kuzuia maradhi ya UKIMWI na mengine makubwa yakiwemo Saratani
kwa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment