Waziri wa Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakata wachezaji wa timu ya soka ya
wanawake chini ya umri wa miaka 17 kucheza kombe la dunia
litakalofanyika nchini India mwaka huu, huku akiipa jina la Serengeti
Girls na kutaka waendeleze kipigo kwa mchezo wa marudiano wa kufuzu
kombe la dunia dhidi ya Botwana utakaofanyika machi 20, 2022 nchini
Botswana.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Machi 11, 2022
baada ya kuitembelea timu hiyo iliyo kaa kambini Zanzibar tangu
Februari 23, 2022 ambako inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa
marudiano na timu ya Botswana baada ya kuichabanga timu hiyo mabao saba
kwa nunge.
Ameongeza kuwa watanzania wana matarajio makubwa na
timu hiyo kuwa italinda na kutetea heshima Taifa letu ndiyo maana
ameamua kuipa jina la Serengeti kwa kuwa hifadhi hiyo ina heshima kubwa
duniani kubwa.
“Nimeamua kuwapa jina hilo la Mbuga yetu ya
Serengeti kutokana na ukweli kuwa Mbuga yetu inaheshimika ni matarajio
yetu kuwa mtaendelea kutuheshimisha hata katika mchezo unaokuja hivi
karibuni na wapinzani wetu Botswana”amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Mhe.
Mchengerwa ametumia ziara hiyo kuzungumza na wachezaji na kuwapa hamasa
na mbinu mbalimbali za kuweza kushinda na kuwataka wawe nidhamu ya
kutosha, umahiri na moyo wa kujituma wakiwa mchezoni.
Aidha,
Mhe. Mchengerwa amezungumza na benchi la ufundi pamoja na viongozi wa
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na na Shirikisho la Soka la
Zanzibar (ZFF) na kuwataka kuendelea kushirikiana kikamilifu na Serikali
katika kuendeleza mchezo wa soka kwa kuzingatia weledi wa mchezo huo.
Amepongeza
hatua ya ushirikiano uliopo baina TFF na ZFF ambapo amesema ushirikiano
unapaswa kuendelezwa katika michezo yote ili kuendelea kuibua na kunoa
vipaji vya wachezaji ambao wataliwakilisha taifa la Tanzania kimataifa.
“Nimefarijika
sana kuona vijana wetu wamekaa kambini hapa Unguja tangu tarehe 23
Februari 2022 huu ndio uzalendo na ushindi kwenye sekta zetu”.
Amefafanua Mhe. Mchengerwa.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, March 11, 2022
Home
MICHEZO
Waziri Mchengerwa -Timu ya Wanawake U17 kuitwa Serengeti Girls, aifunda, ataka kuibamiza tena Botswana iingie kombe la dunia.
Waziri Mchengerwa -Timu ya Wanawake U17 kuitwa Serengeti Girls, aifunda, ataka kuibamiza tena Botswana iingie kombe la dunia.
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment