A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 14, 2022

Wanajeshi Wengine Wafunga Ndoa Vitani Ukraine

 

Wanajeshi wawili wa Ukraine ambao walikutana vitani mwaka 2015, wameamua kufunga ndoa wakiwa uwanja wa vita ambapo vikosi vyao vinaendelea kupambana vikali na majeshi ya Urusi.

Wanajeshi hao ambao kwa sababu za kiusalama majina yao hayajawekwa wazi, walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2015 wakati wa vita vya Donbas ambapo miaka saba baadaye, hatimaye wameamua kufunga ndoa.

Ndoa hiyo imefungwa katika Mji wa Brovary, nje kidogo ya Mji Mkuu wa Kyiv huku wakieleza kwamba wanapitia katika wakati mgumu kutokana na vita hivyo.

Sherehe ndogo ya ndoa hiyo, imefanyika Jumapili ya Februari 13, 2022 katika Hospitali ya Brovary ambapo wamefunga ndoa wakiwa katika nguo zao za kijeshi na kusindikizwa na wanajeshi wenzao kadhaa.

“Kuna wakati mgumu zaidi mbele yetu kwa hiyo tumeamua kufunga ndoa sasa,” alikaririwa bwana harusi wakati wa sherehe hiyo.

Baada ya ndoa kufungishwa, maharusi waliungana na wanajeshi wenzao na baadhi ya mashuhuda, kucheza muziki wa bandura ambao ni maarufu zaidi nchini Ukraine.

Hatua ya wanajeshi hao, inakuja siku chache baada ya wanajeshi wengine, Lesya na Valeriy nao kuamua kufunga ndoa wakiwa uwanja wa vita ambapo walisindikizwa na wenzao waliokuwa na silaha begani kukamilisha hatua hiyo muhimu katika maisha yao.

Siku chache zilizopita, Meya wa Jiji la Kyiv, Vitali Klitschko aliwatembelea wanandoa wawili waliofunga ndoa wiki iliyopita, Lesya na Valeriy ambao baada tu ya kufunga ndoa, waliendelea na mapambano dhidi ya uvamizi wa majeshi ya Urusi.

Wakati hayo yakiendelea, majeshi ya Urusi yanazidi kusonga mbele ambapo sasa yameukaribia mji wanajeshi hao walipofungia ndoa, Brovary ambapo maafisa nchini humo wanakadiria kwamba magari zaidi ya 70 na wanajeshi takribani 300 wa Urusi, wanaukaribia mji huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages