Mwanamume mmoja katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya anauguza majeraha baada ya kung’atwa uume wake na mwanamke.
Kulingana na taarifa zilizotolewa kuhusu tukio hilo, mwanamume huyo aliyefahamika kwa jina moja la Anthony alisikia kelele za ugomvi nyumbani kwa jirani yake ambapo ndugu wawili walikuwa wakipigana, alifika pale na kujaribu kuwatenganisha.
Mwanamke ambaye alikuwa akigombana na kaka yake vita hivyo aliachana na ugomvi huo kisha kumrukia jamaa huyo aliyefika kusuluhisha mzozo kisha kumng’ata nyeti zake na kumsababishia majeraha makubwa.
Mwathiriwa alisema alijaribu kuvumilia maumivu hayo lakini hakuweza, akamjulisha jirani yake ambaye alimkimbiza hospitalini.
“Yule dada alikuwa anapigana na kaka’ke, alipomwachia kaka yake alikuja na kuning’ata, moja kwa moja alinishukia na sikuweza kukabiliana naye, nilijaribu kujizuia na maumivu lakini yote yalishindikana,” alisema Anthony.
No comments:
Post a Comment