Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amewataka Watanzania kuachana na dhana ya unyonge kwani kauli ya unyonge inalemaza.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 14, 2022 katika Ukumbi wa JNICC, Posta jijini Dar es Salaam, wakati akitolea ufafanuzi kuhusu upandaji wa vifurushi vya simu, ambavyo vimeonekana kulalamikiwa na Watanzania wengi.
“Niwaombe Watanzania tuondoke kwenye kulalamika, unajua hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge inatulemaza, nataka niwaombe tuwape muda TCRA, lakini hebu tuondoke kwenye badhi ya mambo ambayo tunadanganyana,” amesema Waziri Nape.
No comments:
Post a Comment