A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 21, 2022

Vijana watakiwa kubadilika kusoma vitabu vyenye utatuzi wa changamoto

 Vijana nchini wametakiwa kubadilika kifikra kwa kusoma vitabu mbalimbali vitakavyowajenga katika maadili na kufanya Taifa liwategemee katika kuleta maendeleo .

Kusoma vitabu kusoma vitabu kutafanya kuondokana na utumwa wa kifikra na kuwa vijana wanaoweza kusimamia ndoto zao za maisha huku wakikombolewa na umasikini.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu chake Kiitwacho Vijana wa Kikristo na Changamoto na Utatuzi Wake, Mwandishi wa Kitabu hicho Mwijarubi Mwijarubi amesema kuwa vijana wengi hawachukui muda kusoma na kujifunza mambo mengi ya kukabiliana na maisha na changamoto zake hivyo kupitia kitabu hicho kitaweza kuwasaidia kupambana nazo na kwa kujenga fikra mpya zinaweza kuleta suluhu katika maisha yao.

“Kitabu hiki kimegawanyika katika changamoto za vijana katika makundi makuu manne ambayo yamefafanuliwa kwa ufupi katika Afya,Uchumi, Utandawazi na Mahusiano”. Amesema Mwijarubi.

Kwa upande wake Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Richard Hananja amewataka vijana kutumia kitabu kama sehemu ya kutatua na kupambana na changamoto za maisha ambazo wakati wa wa sasa wana vitu vingi vinavyowazunguka

Katika uzinduzi huo Mgeni rasmi wa kitabu hicho Lello Mmasy ambaye ni Mwandishi wa vitabu kama “Mimi na Rais” pamoja na Chochoro za Madaraka amesema kwamba kila kijana atakayesoma kitabu hicho kitambadilishia mtanzamo wake katika maisha yake na kuongeza kuwa vijana ili waweze kubadilika kifikra lazima wasome vitabu kama hivyo ambavyo vina majawabu ya changamoto za vijana.

Amesema kuwa maisha yanabadilika kwa kasi hivyo vijana wanatakiwa kuleta matokeo chanya ya kufanya vitu tofauti ya kubadilika katika nyanja mbalimbali za kusaidia maisha yao yaende kwa kufanya vitu tofauti.

Aidha amesema kitabu hicho amekisoma na kugundua kipo katika kubadilisha vijana ambapo wanatakiwa kusoma na kuelewa kilichomo na maisha yao katika kutafuta ufumbuzi.

Mgeni rasmi Lello Mmassy akiwa na wadau Kitabu cha Vijana wa Kikristo ,Changamoto na Utatuzi Wake  baada ya kuzinduliwa kwa kitabu hicho katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Lello Mmassy watatu kutoka kushoto  na akizindua   kitabu cha Kitabu cha Kikristo,Changamoto na Utatuzi Wake katika hafla uzinduzi huo  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Kitabu cha Vijana wa Kikristo ,Chagamoto na Utatuzi wake Mwijarubi Mwijarubi akizungumza kuhusiana na dhamira ya kitabu hicho kwa vijana kitavyowesha kuwakomboa kifikra ,kilichozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi wa Kitabu cha Vijana wa Kikrisro ,Changamoto na Utatuzi Wake Lello Mmasy qkizungumza wakati wa Uzinduzi wa kitabu hicho kilichoandikwa na  Mwandishi Mwijarubi Mwijarubi kilichozinduliwa  jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages