MKURUGENZI
wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, TARI Naliendele Dkt.Fortunus Kapinga
amesema kuwa tekolojia ya Mtwara inaruhusu wakulima wa Mtwara kulima
mazao mengi yakiwemo mazao ya bustani, jamii ya kunde na nafaka bila
kuathiri kilimo cha zao la korosho.
Hivyo wanaweza kujiongezea kipato kutoka kwenye mazao hayo badala ya kutegemea zao la korosho peke yake.
Dkt.Kapinga
alisema kuwa mahitaji ya kiikolojia ni mojawapo ya sababu zinazowafanya
washauri zao fulani lipandwe wapi, lini na vipi.
Dkt.Kapinga
ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi kutoa Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo cha Kilimo Borigaram - Kigamboni
walioko kituoni hapo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Field Practical)
katika taasisi hiyo.
Wakizungumzia
tafiti za kilimo cha mboga na matunda (hotculture) wanafunzi hao
wamesema wameshangaa kuona migomba ikistawi na kuzaa kwa wingi na
kudai kuwa wakazi wa Mtwara wanaweza kutengeneza kipato kikubwa wakati
wakisubiri mavuno ya mazao mengine kama vile Korosho na Ufuta.
No comments:
Post a Comment