WAKATI
wakulima wakijiandaa kuanza msimu wa kilimo kwa mazao mbalimbali,
Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewahimiza
wakulima kutumia mbegu zilizothibitishwa ubora.
Sambamba
na kukaguliwa na taasisi hiyo ili kupata mazao yenye ubora na
kuhakikisha wanapata risiti ili likibainika tatizo iwe rahisi kuwabaini
wauzaji feki wa mbegu.
Tayari
TOSCI imeshakagua ubora wa mbegu katika kipindi cha mwaka 2020-2021,
lengo likiwa ni kupambana na wauzaji wa mbegu zisizo na ubora kabla
wakulima hawajazitumia kupanda.
TOSCI
imekuwa ikifanya ukaguzi wa mbegu kila mwaka kabla ya misimu ya kilimo,
lengo likiwa ni kupambana na wauzaji mbegu feki na wamekuwa wakiufanya
ukaguzi huo kwenye maduka,maghala ya kuhifadhia mbegu.
Pia
kuangalia wafanyabiashara halali wa mbegu ambao wanatakiwa kuwa na
vibali vya kuuzia mbegu na kukagua maghala ya wafanyabiashara wa mbegu
ama wazalishaji wa mbegu.
Ukaguzi wa TOSCI ni wa muda wote hata kama ni nje ya misimu ya kilimo huku kaguzi zao zikiwa za kushtukiza.
Vitu
muhimu wanavyoviangalia kwenye maghala ni pamoja na kutambua mbegu
zilizofanyiwa majaribio ya ubora wa maabara kwa kipindi cha miezi saba.
Kila baada ya miezi saba mbegu inatakiwa kufanyiwa majaribio kutokana na Sheria ya Mbegu ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake.
Hivyo
mbegu ambazo zimepita muda huo wa miezi saba na hazijafanyiwa majaribio
zinafungiwa na zitatakiwa kufanyiwa majaribio na kama zikifanyiwa
majaribio na ikabainika hazina ubora zitateketezwa.
Katika
uhifadhi mbegu zinatakiwa kuhifadhia katika mazingira yenye ubora, kuwa
na uhalali kama amesajiliwa na TOSCI kwa kuwa sheria inataka anayefanya
biashara ya mbegu lazima asajiliwe na TOSCI ambapo sheria na taratibu
inataka mtu yeyote kabla hajajiingiza kwenye biashara ya mbegu lazima
apate mafunzo kutoka TOSCI na kusajiliwa.
Katika
majaribio ya uhalisia wa mbegu zilizoko katika uzalishaji katika
kipindi cha mwaka 2021, TOSCI iliandaa majaribio ya kutathmini uhalisia
wa mbegu zilizoko katika uzalishaji ambapo jaribio Hilo lilihusisha
sampuli za mbegu za mazao ya madaraja aina tofauti.
Mazao
hayo ni alizeti sampuli 53,ufuta sampuli 13,mtama sampuli 8,mpunga
sampuli 11,maharage sampuli 33 na mahindi sampuli 253 kati ya majaribio
hayo mbegu za hybrid zikiwa 232 na OPV 21.
Fatuma
Nassoro ni mtafiti wa mbegu daraja la 2 wa TOSCI anasema, katika
majaribio ya utambuzi wa aina mpya za mbegu katika kipindi cha mwaka
2021 taasisi ilipokea jumla ya maombi 98 kwa ajili ya kufanya majaribio
ya utambuzi wa aina mpya za mbegu za mazao mbalimbali ambapo jumla ya
majaribio 51 yalifaulu,4 hayakufaulu na 43 yanaendelea kuchukuliwa
takwimu.
Aidha,
Mtafiti Fatuma alisema katika kipindi cha mwaka 2021 TOSCI imepokea
maombi 20 kwa ajili ya kufanya majaribio ya umahiri wa aina mpya za
mbegu.
Mazao
hayo ni pamoja na mahindi 10,maharage 3,uwele wa malisho1,Mtama wa
malisho 3,nyasi za malisho 2,na alizeti 1,huku TOSCI ikiendelea na
upandaji wa majaribio hayo katika kanda na maeneo tofauti kama
inavyoainishwa katika kanuni ya mbegu.
Fatuma
anasema pia katika kipindi hicho hicho cha 2021 taasisi iliendelea
kuhudumia,kuchukua takwimu,kuzichakata na kuandaa taarifa za majaribio
saba ya NPT ya msimu wa kilimo kwa mwaka 2020/2021 yaliyopandwa katika
mikoa ya Njombe, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Songwe, Mbeya, Iringa,
Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa wa Lindi.
Mtafiti
huyo anasema taarifa za majaribio hayo zinahusisha aina mpya za mazao
ambazo ni mahindi 9,ngano 4,ulezi 2, na choroko 2,huku taarifa ya
majaribio hayo ikiwasilishwa katika kikao cha 21 cha kamati ya kitaalamu
ya majaribio ya umahiri ya kitaifa ya aina mpya za mbegu (NPT-TC).
Katika
uchukuaji sampuli za mbegu kwenye maghala mwaka 2021 jumla ya sampuli
2691 kutoka kwenye mafungu ya mbegu (seed lot) yenye uzito wa MT
29,205.2 zilifanyiwa vipimo vya maabara TOSCI Morogoro,Arusha,Njombe na
Mwanza.
Kati
ya sampuli zilizofanyiwa vipimo hivyo sampuli 2372(88.1%)zilifaulu
wakati sampuli 255 sawa na asilimia 9.5 hazikufaulu na sampuli 64 sawa
na asilimia 2.4 zilikuwa zikiendelea kufanyiwa vipimo vya maabara.
Katika
kipindi cha mwaka 2021 jumla ya sampuli 135 zenye MT 82.7za mbegu (QDS)
zilijaribiwa maabara ya TOSCI ambapo kiasi hicho cha mbegu ni sawa na
asilimia 5 ya mbegu zote zilizozalishwa nchini kwa mwaka 2021.
Katika
mwaka 2021 TOSCI pia ilikagua usajili wa mbegu kwa wafanyabiashara
pamoja na makampuni ambapo makampuni ya mbegu yalibainika
kusajiliwa,pamoja na wafanyabiashara wa maduka 196.
Katika
kipindi hicho hicho pia TOSCI iliendesha zoezi la ukaguzi wa maduka ya
mbegu katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mtwara, Lindi, Dar es Salaam,
Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe,Tanga na Pwani.
TOSCI
iliweza kukagua maduka 367 ambapo kati ya maduka hayo 165 ndiyo
yaliyokuwa yamesajiliwa huku 191 hayakusajiliwa na maduka 11 yalifungiwa
kwa kosa la kupata mafunzo, lakini hawajaomba kibali cha kuuza mbegu.
Kutokana
na hatua hiyo wafanyabiashara wote wametakiwa kufanya biashara ya mbegu
kwa kufuata Sheria ya Mbegu ya mwaka 2003 iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2014 pamoja na kanuni zake za mwaka 2017.
Mara
baada ya marekebisho ya Sheria ya Mbegu ya mwaka 2014 pamoja na kanuni
zake za mwaka 2017, TOSCI ilipewa mamlaka ya kuteketeza mbegu zilizoisha
muda wake au zenye viwango duni ama dhaifu vya ubora.
Katika
kipindi cha mwaka 2021 TOSCI iliteketeza jumla ya tani za ujazo 279.6
za mbegu,mbegu hizo ziliteketezwa katika Kanda ya Kati na Kaskazini
kutokana na mbegu hizo kushuka ubora wake wa uotaji.
UTOAJI WA VIBALI
Katika
kipindi cha mwaka 2021 jumla ya vibali 2,333 vya uagizaji mbegu nje ya
nchi vilitolewa na TOSCI kwa vituo vya utafiti,makampuni ya uzalishaji
mbegu na wauzaji wa mbegu,mbegu hizo zilikuwa kwa ajili ya
biashara,majaribio na uzalishaji ambazo kwa pamoja zilikuwa na uzito wa
MT 24,246.4 vile vile vibali 12 vya kuuza mbegu nje ya nchi vilitolewa
kwa mbegu zenye uzito wa MT 501.8.
TOSCI
iliweza kuendesha mafunzo kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya mbegu
kuhusu Sheria na kanuni za mbegu pamoja na udhibiti wa ubora wa mbegu
jumla ya wafanyabiashara ya mbegu 752 walipewa mafunzo.
No comments:
Post a Comment