Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Mkongo wilayani Namtumbo wakichota maji
katika kituo kimojawapo kilichojengwa na wakala wa usambazaji maji
safi na usafi wa mazingira kupitia mradi mkubwa wa maji uliotekelezwa
na Serikali kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa kijiji cha Mkongo na
Nahimba.
Fundi sanifu wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)wilaya
ya Namtumbo mkoani Ruvuma Salum Nachundu kushoto,akimtwisha ndoo ya
maji mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Mkongo Zakia
Simkala,baada ya Ruwasa kufikisha huduma ya maji kwa ajili ya matumizi
ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Tenki la maji lenye uwezo wa kuchukua takribani lita 100 linaloendelea
kujengwa katika mradi wa maji kijiji cha Masuguru wilayani Namtumbo na
Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira( Ruwasa) ambalo
litakapokamilika litahudumia wakazi wapatao 3264 wa kijiji hicho.
===== ======= = ======= ========
WIZARA
ya maji kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira
vijijini(Ruwasa)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,imeanza kutekeleza
miradi ya maji katika vijiji mbalimbali ambavyo kwa muda mrefu havikuwa
na huduma hiyo.
Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Salum
Nachundu, alitaja miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji Mkongo
Gulioni-Nahimba uliotekelezwa chini ya Programu ya maendeleo ya sekta ya
maji(WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira
vijijini(RWSSP).
Alisema, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka
2017na mkandarasi Kipera Contractors ambaye alitakiwa kukamilika kazi
mwaka 2020,lakini alishindwa kukamilisha kazi kutokana na changamoto
mbalimbali ikiwamo uwezo mdogo wa kiufundi na fedha.
Nachundu
alieleza kuwa,baada ya Serikali kukatisha mkataba na mkandarasi, mradi
huo umekamilishwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira
vijijini(Ruwasa) kwa njia ya force akaunti ambapo kwa sasa umekamilika
na wananchi wanapata huduma.
Kwa mujibu wa Nachundu,mradi wa
Mkongo gulioni-Nahimba ulisanifiwa kuhudumia wakazi 8,007 katika vijiji
hivyo ambapo awali gharama ya mradi ilikuwa Sh.2,069,975,521,hata hivyo
zilipungua hadi Sh.1,451,531,411 baada ya Ruwasa kutekeleza mradi huo
kwa kuwatumia mafundi wa kawaida.
Aidha, alitaja mradi mwingine
unaotekelezwa ni katika kijiji cha Masuguru ambao unatarajia kuhudumia
wananchi wapatao 3,264 na gharama za mradi huo ni Sh.402,000,000.
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Gloria Nziku alisema,mradi wa
maji katika kijiji cha Msuguru unatekelezwa chini ya program ya malipo
kwa matokeo na ulianza kutekelezwa mwezi Agosti mwaka 2021 na unatarajia
kukamilika tarehe 30 mwezi huu.
Nziku,ameishukuru wizara ya
maji kutoa fedha na serikali ya kijiji na wananchi,kwa ushirikiano
mkubwa waliotoa wakati wa utekelezaji wa mradi huo ambao hadi sasa
umefikia asilimia 85.
Alisema,mradi utakapokamilika jumuiya ya watumia maji Masuguru ndiyo watakuwa wasimamizi wakuu na waendeshaji wa mradi huo.
Amewataka viongozi wa jumuiya na wananchi kuhakikisha wanalinda
miundombinu ya mradi ili uendelea kufanya kazi kama ilivyokusudiwa na
serikali.
Mkazi wa kijiji hicho Dolfina Chowo
alisema,wanachangamoto kubwa yam aji safi na salama ambapo wanatumia
maji ya visima vya kupampu na wakati mwingine maji ya visima na mito
iliyopo kando ya kijiji hicho.
Alisema, sasa wana matumaini
makubwa ya kuondokana na kero hiyo baada ya serikali kupitia wakala wa
maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kuanza kutekeleza mradi wa maji
ya bomba ambao umeanza kuleta matumaini makubwa kwao
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, March 17, 2022
SHILINGI BILIONI 2 KUMALIZA KERO YA MAJI MKONGO NA MASUGURU
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment