Supastaa wa muziki Bongo anayetamba na EP yake ya FOA, Diamondp Platnumz kwenye mahojiano na Wasafi FM leo Machi 14, 2022 amefunguka kuwa anaweza kufanya show ya pamoja na staa mwenzake Alikiba na alishawahi kuuomba uongozi wake.
Diamond amebainisha hayo kupitia kipindi cha The Switch ambapo amesema yeye hana noma na mtu.
“Nishapigia simu Menejimenti yake tukitaka tuandae show, nilishamwalika kwenye show zangu kabla hata ya Wasafi Festival, mimi sina noma yaani fresh tu” amesema Diamond.
Pia amefunguka kuwa kuna mawazo Watanzania tuyafute, ili uwe mkubwa lazima ugombane na mtu.
“Ila kuna mawazo ambayo Watanzania tunatakiwa tuyafute, ili wewe uonekane mkubwa lazima ugombane na mtu, mimi sina noma halafu kila mtu namuheshima kwa upande wake. Ila mtu akitaka kunivunjia heshima, usitake kunibadilisha, unitotoshe, hapo ndio sikubali, kila mtu achukue heshima yake,” amesema Diamond.
No comments:
Post a Comment