Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Jerry
Silaa akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea Hifadhi
ya Msitu wa Asili wa Amani.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mwenyekiti wa
Kamishna
wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos
Silayo akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo
NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC)
imeishauri serikali kuangalia sheria ya usafirishaji wa viumbe hai nje
ya nchi ilivyowaathiri wafugaji wa vipepeo wa Amani Wilaya ya Muheza
mkoani Tanga
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo,
Jerry Silaa wilayani Muheza wakati wa ziara ya kamati hiyo
ilipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani.
Amesema
Serikali ipitie sheria hiyo na kuangalia namna ambavyo wananchi
waliokuwa wanafuga vipepeo na kuwauza nje nchi kwa ajili ya kujipatia
kipato wameathirika.
"Serikali ilitoa katazo baada kuingia
dosari ya kusafirisha viumbe wengine zaidi ya vipepeo, hivyo
tunapendekeza ipitie sheria hiyo ili kuendeleza ufugaji wa vipepeo kwa
wananchi na kujiongezea vipato vyao," amesema Silaa.
Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilijionea miradi mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo inayotekelezwa na TFS katika msitu huo.
"Tumejionea
mambo mengi tukiwa katika hifadhi hii, aina mbalimbali za miti ambayo
inapatikana hapa, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na njia za
watembea kwa miguu na majengo na tumefurahishwa," amesema Silaa.
Aidha,
amesema wajumbe wa kamati hiyo wameridhishwa na matumizi ya fedha za
Serikali zilizotolewa kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya barabara
na majengo.
Awali akizungumza wakati wa Kamati hiyo, Kamishna wa
Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo
alisema maelekezo ya wizara watakwenda kufanyia kazi na suala la
kusafirisha viumbe hai nje wameelekeza jambo hilo lifanyiwe mapitio
kuona namna ambavyo suala la vipepeo vinaweza kufanyiwa utaratibu wa
kisheria ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kufaidika na utaratibu wa
kufuga waone tija ya kushiriki kwao kwenye uhifadhi wa rasilimali za
misitu kwenye eneo hilo.
“Tunahaidi kwamba tutakwenda kulifanyia
kazi serikali yetu ni sikivu inaongozwa ya Rais wetu Samia Suluhu na
tunaamini jambo hili litafanyiwa kazi na bunge wakati wote limekuwa
likishauri kwenye masuala mbalimbali hivyo tunalichukua na katibu mkuu
wetu atafikishiwa taarifa hizo kwa ajili ya utekelezaji”Alisema
Hata
hivyo alisema wanaishukuru kamati kuwatembelea na kukagua miradi
inayotekelezwa na serikali katika kufadhiliwa na fedha za kupunguza
makali ya uviko 19 ambapo mradi umejengwa eneo la kuingilia eneo la
hifadhi hiyo.
Alisema pia kuna mradi wa barabara ikiwemo wa
kuboresha nyumba na makazi kwa ajili ya watafiti au watalii kwenye fedha
za uviko ambapo msitu huo ulitengewa Sh.Million 502 kati ya shi Bilioni
4 ambazo TFS walipewa kutekeleza miradi kwenye msitu 11.
Naye
kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo aliishukuru
kamati hiyo kwa kuliona suala la vipepeo na walichobakia ni serikali
kulifanyia utekelezaji vipepeo wilayani humo inaingia mapato kwa
serikali ni shughuli ambazo ilikuwa inawasaidia kiuchumi pia wananchi.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 21, 2022
PIC YAISHAURI SERIKALI KUANGALIA UPYA KATAZO LA USAFIRISHAJI WA VIPEPEO NJE YA NCHI
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment