A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 14, 2022

Mwandishi wa Marekani Auawa Ukraine

 

MWANDISHI wa habari wa Shirika la Habari la New York Times la Marekani, Brent Renaud amepigwa risasi na kuuawa akiwa katika majukumu yake ya kuripoti vita vinavyoendelea nchini Ukraine katika Mji wa Irpin uliopo Kaskazini Magharibi mwa Kyiv, huku mwingine akijeruhiwa vibaya.

Daktari wa upasuaji anayefanya kazi ya kujitolea nchini Ukraine kuwatibu watu wanaojeruhiwa vitani, Danylo Shapovalov ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mwandishi huyo alipoteza maisha papo hapo huku mwenzake akikimbizwa hospitali.
“Alipigwa risasi shingoni, akapoteza maisha palepale, tulijaribu kumsaidia mwenzake kwa kumpa huduma ya kwanza pamoja na raia wa Ukraine na baadaye wamepelekwa hospitali,” amekaririwa Shapovalov.

Shapovalov ameiambia AFP kwamba mwandishi huyo na mwenzake, walikuwa ndani ya gari wakiwa na raia mmoja wa Ukraine, waliposhambuliwa kwa risasi na makombora na majeshi ya Urusi.

Maafisa nchini Ukraine, wamelaani shambulio hilo ingawa bado hawajatoa taarifa kamili zaidi ya kueleza kuwa gari lililowabeba waandishi wawili wa habari na raia mmoja wa Ukraine, limeshambuliwa na majeshi ya Urusi.

Nyaraka zilizokutwa kwenye mwili wa mwandishi huyo wa habari, zinaonesha kwamba alikuwa na umri wa miaka 50 na alikuwa akifanya kazi na shirika hilo kuripoti habari za vita pamoja na kurekodi ‘docomentary’ za hali ilivyo nchini Ukraine.

Mkurugenzi wa The New York Times, Cliff Levy amethibitisha kumtambua mwandishi huyo ambaye pia ni mpigapicha na kumueleza kwamba alikuwa mfanyakazi aliyeipenda kazi yake na mwenye ubunifu wa hali ya juu.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema kwamba mpaka anafikwa na mauti, mwandishi huyo alikuwa ameacha kulifanyia kazi shirika hilo na wala hakutumwa Ukraine kwa ajili ya kuripotia chombo hicho cha habari.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages