Siku
ya Machi 14, 2022 nilipata wasaa wa kumsoma Baba Askofu Emmaus
Mwamakula katika matini iliyokuwa na aya karibu ya 16 juu ya mgogoro
baina ya waliokuwa wanafunzi wa Azania na Tambaza kati ya mwaka 1993 na
1994 jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa na mimi nilikuwa miongoni
mwa wanafunzi hao wakati huo na nami nainyanyua kalamu yangu kuandika
yale ambayo nitajaliwa kuyakumbuka huku mengine nikiwasiliana na
wenzangu tuliokuwa nao wakati huo ambapo nitayaandika katika matini
mfululizo.
Kabla sijaingia katika mgogoro wenyewe wa siku hiyo
naomba msomaji wa matini hii nadhani ni vizuri mno kuzifahamu vizuri
shule hizi mbili Azania na Tambaza kihistoria. Tangu enzi zilikuwa ni
shule za wavulana tu lakini baadaye Tambaza kidato cha tano na sita
waliingizwa wasichana.
Azania walikuwa na urafiki na Jangwani,
nashukuru hili hata Baba Askofu Mwamakula amelitaja, Tambaza walikuwa na
urafiki na Zanaki. Bahati nzuri ya Azania walikuwa majirani mno na dada
zao shule rafiki Jangwani, wakati Tambaza walikuwa mbali kidogo na dada
zao rafiki shule ya Zanaki.
Ujirani wa Azania na Jangwani
ulisaidia mno wanafunzi wa Azania kutokuwa watundu zaidi kwani mara zote
walikuwa wakiwaona wanafunzi wa Jangwani na sketi zao za rangi chungwa
ambazo ziliwavutia mno vijana wa Azania hata sie tuliokuwa tukisoma
Tambaza wakati huo.
Nakumbuka hata bweni la wanafunzi wa A level wa Jangwani lilikuwa katika viwanja vya Azania wakati huo
Nikirudi
nyuma zaidi kuanzia mwaka 1990 shule kadhaa za umma za kutwa za Dar es
Salaam zilitakiwa kuwapokea wanafunzi wengi ili kutoa nafasi ya
wanafunzi wengi zaidi wa mkoa huu kupata elimu ya sekondari, kwa hiyo
wakati huo kukawa na wanafunzi wengi wa kidato cha kwanza na kukawa na
makundi mawili yenye mikondo kumi na miwili na kila mkondo ulikuwa na
wanafunzi 40 jumla kuu ilikuwani wanafunzi 480 kwa kidato cha kwanza
tangu mwaka huo 1990.
Wanafunzi hawa 480 wa Azania na 480 wa
Tambaza na shule zingine waliofaulu pamoja wakiwa msingi walisoma
pamoja, walipofaulu walitenganishwa tu na shule hizo. Kama ukiwafuatilia
tangu wadogo pengine mafundisho ya kipaimara kanisani, kupokea
Kipaimara hicho walipokea pamoja, madrasa walisoma pamoja.
Wengine
walikuwa ndugu wa damu, kaka alikuwa Tambaza na mdogo mtu alikuwa
Azania. Hali hii ilikuwa hivyo hivyo kwa Zanaki , KIusutu , Kibasila ,
Forodhani na Jangwani.
Swali la kulijibu ilikuwaje hawa
wanafunzi walisoma pamoja shule ya msingi, waliokuwa wakisoma pamoja
kipaimara na walisoma pamoja madrasa wakaja kuwa maadui hadi wakipigana
kwa kutumia mabomu ya petrol kama alivyosimulia Baba Askofu Mwamakula?
Kwa
miaka mingi shule ya Tambaza ilikuwa ya wanafunzi watundu, wachangamfu,
wapenda utani, wacheshi na vituko vya hapa na pale huku pia wakitazamwa
kama magangwe wa mjini. Kwa kuwa walipokuwa waksoma Tambaza hawakuwa
jirani na wasichana kama Azania, ndiyo maana vitendo hivyo vya utundu
uliovuka mipaka uliongezeka.
Japokuwa walikuwa watundu hivyo
walifanya vizuri kitaaluma lakini wapo wanafunzi ambao walivuka mipaka
ya tabia hizo mbaya huku walimu wa shule na serikali wakijahidi
kuyafanyia kazi.
Japokuwa shule hizi zilipokea wanafunzi wengi
kwa upande wake serikali ilijitahidi kuwapatia chai na chakula cha
mchana wanafunzi wote lakiai changamoto moja kubwa ilikuwa ni usafiri wa
wanafunzi hapo ndipo shida ilipoanza.
Nakumbuka makondakta
walikuwa vijana ambao walikuwa wamemaliza darasa la saba wengine kidato
cha nne hawa walishindana mno kwenye usafiri na wanafunzi wa Tambaza
wakati wakienda shule au kurudi nyumbani.
Wanafunzi wa Tambza
wakiwa katika makundi kulingana na wanapotokea mathalani Mkaundi
Magomeni, Tandika, Ubungo, Mwananyamala, Kijitonyama, Mwenge, Kawe na
hata Mbagala na wakienda shuleni pamoja na kurudi pamoja.
Makondakta
walikuwa wakitafuta faida ya biashara zao sasa linapokuja kundi la
wanafunzi wa Tambaza wapande wote hiyo ni hasara kwao, hapo ndipo ngumi
zilipotokea.
Kutoka na hilo CCM hasa hasa Umoja wa Vijana wa
wakati huo ulijaribu kulitatua na kuja na mradi wa mabasi ya wanafunzi
ambapo wanafunzi wote tulipewa makadi ya kuchangia mradi huo na mradi
huo kuanza. Chini ya UVCCM ya John Guninita na akiwamo Wiliam Lukuvi
japokuwa baadaye mradi huu ulikufa. Huku yakitumiwa mabasi ya mashirika
ya umma kubeba wanafunzi kama kuokoa jahazi.
Yale mkundi ya
kupambana na makondakta yaliwapa nafasi wanafunzi wengi wa Tambaza
kujifunza michezo kadhaa ikiwamo kubeba vyuma karate, ngumi nakadhalika
hili wawe magangwe wa kweli.
Kwa wale wanaozifahamu siasa za
Tanzania wakatihuo wapigania uhuru wengi walikuwa hapa nchini na familia
zao. Watoto wao wakisoma katika mifumo ya elimu ya Tanzania wengine
walipata elimu hadi ya Chuo Kikuu.
Baadhi yao walisoma Tambaza
kwa kidato cha Tano na cha Sita, kwa kuwa walikuwa wapigania uhuru
waliambukiza zile mbinu za kivita za awali kama mabomu ya petrol na
kutumia mawe kwa wanafunzi wenzao na palipokuwa panatokea vurugu
mbalimbali kama ya Azania na Tambaza, Tambaza na JKT Mgulani, Tambaza na
Kinondoni Muslimu na ugomvi Tambaza na Makondakta na hata Kuvunjwa kwa
ukuta wa shule ya Msingi Muhimbili.
Ujuzi huu ulitumika katika
ugomvi binafsi mathalani wa kuwagombania wasichana kama ulivyokuwa huu
mgogoro wa Azania na Tambaza hadi kuumizana na kuharibu mali za umma.
Serikali
ya wakati huo chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi haikukaa kimya bali
walifuatilia mno jambo hilo chini ya Waziri wa Elimu wakati huo Profesa
Philimon Sarungi , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ditopile Mzuzuri na RPC
Dar es Salaam Typhone Maji na hata baadaye RPC Mwinyi Dadi Ally.
Naomba
kwa leo niishie hapo, matini ijayo nitaendelea zaidi kuusimulia mgogoro
mmoja baada ya mwingine hadi shule hii kufungwa na baadaye kuwahamisha
wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili pamoja na baadhi ya wanafunzi
wa kidato cha tatu na cha nne.
Nakutakia siku njema
makwadeladius@ gmail.com
0717649257
Post Top Ad
Your Ad Spot
Tuesday, March 15, 2022
MGOGORO WA AZANIA NA TAMBAZA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment