KAMISHNA msaidizi wa ardhi Mkoa
wa Pwani amekabidhi mashauri yapatayo 68 katika baraza la ardhi na
nyumba la Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa wadaiwa sugu ambao
hawataki kulipa kabisa kodi ya ardhi kwa kipindi kirefu ili waweze
kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye
vitendo kama hivyo vya kuikosesha serikali mapato kwa makusudi.
Akizungumza
maara baada ya kukabidhi mashauri hayo Kamishna msaidizi wa ardhi Mkoa
wa Pwani amebainisha kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wadaiwa sugu wa
ardhi hivyo wameamua kulivalia nuga suala hilo ambalo limeonekana kuwa
ni tatizo kubwa katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha na kwamba
wataendelea kuwasaka na kuwafuatilia wadaiwa wote sugu ambao hawataki
kulipa kodi ya ardhi.
Kamishina huyo alibainisha kwamba jukumu
kubwa la serikali ni kuhakikisha kwamba wanasimamia na kukusanya
maduhuli yote ambayo yanatokana na ulipaji wa ardhi hivyo wananchi wote
wanapaswa wanalipa kodi hizo za pango la ardhi ikiwa pamoja na
kuzingatia sehria na taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na
usumbufu.
“Kuna baadhi ya wananchi ambao katika Mkoa wa Pwani
tayari tumewafikia na wengine wameshalipa kwa hiari yao wenyewe bila
usumbufu lakini kuna baadhi yao bado wanakaidi kulipa kwa wakati na hawa
kwa kweli hatuwezi kuwavumilia tutawachukulia hatua ili waweze
kufikisha katika mabaraza ya aradhi na kushughulikiwa na hatua zaidi
ziweze kuchukuliwa,”alifafanya Kamishina huyo.
“Tumeongozana na
jopo la wataalamu mbali mbali wa aradhi ambao tumeweza kuwasilisha
mashauri yapatayo 68 ya wadaiwa sugu katika halmashauri ya Kibaha na
tumeyawasilisha katika baraza la aradhi na nyumba la Kibaha Mkoa wa
Pwani na kwamba zoezi hili bado linaendelea kuwafuatilia wale wote ambao
bado hawataki kulipia kodi ya ardhi,”
Katika hatua nyingine
Kamishina huyo amesema kuwa bado kuna baadhi ya wananchi wanakiuka na
kukaidi kukwepa kulipa kodi ya pango la ardhi na kwamba lengo la
serikali sio kumwonea mtu na badala yake sheria itafuata mkondo wake
ikiwemo mali zao zote kunadiwa pamoja na kufutia hati za miliki na
kuwataka walipe kodi kwa hiari ili kuepukana na usumbufu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa baraza la ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani amebainisha kwamba kwa sasa wamejipanga
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanasuluhisha changangamoto mbali mbali
zinazohusiana na migogoro ya ardhi ili wananchi waweze kupata haki
stahiki kwa wakati kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.
Pia
Mwenyekiti huyo alisema kwamba wao kama baraza wanaataka kuona wananchi
ambao wanakabiliwa na migogoro mbali mbali ya ardhi wanajisuluhisha wao
wenyewe kabla ya kwenda katika baraza hilo lengo ikiwa ni kuleta amani
na utulivu kwa jamii na kwamba wataendelea kutoa huduma kwa kuzingatia
misingi ya haki ambayo inaambatana na sheria na taratibu zote.
Mwonekano wa Kibao kinachoonyesha cha ofisi mpya ya baraza la ardhi na nyumba ya Wilaya ya Kibaha
No comments:
Post a Comment