Meneja wa Dun & Bradstreet Tanzania, Junaid Malik. |
Dar es Salaam, 3 Marchi 2022
- Taasisi ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited
imetangaza kuwa taarifa za mkopaji pamoja na maelezo kwa watumiaji wake,
zitakuwa zinapatikana kwa lugha ya Kiswahili kuanzia sasa. Hapo awali,
taarifa hizi zilikuwa zikipatikana kwa lugha ya Kiingereza tu. Lengo la
Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania kufanya taarifa hizi
kupatikana kwa lugha ya Kiswahili ni kufanya walengwa wake kuzisoma na
kuzielewa vyema.
Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania ni
taasisi inayoongoza kwa kukusanya na kuchakata taarifa zinazomtambulisha
mtu binafsi au kampuni/taasisi kwenda kwa taasisi zinazotoa mikopo kwa
watu binafsi, mashirika pamoja na taasisi za kifedha kutoka vyanzo
mbali mbali na kusizambaza taarifa hizo kwa wateja wake. Taarifa hizi
(Data) husambazwa katika mfumo wa Ripoti ya Taarifa ya Mikopo na utumika
katika kuwezesha wakopeshaji kutathmini ustahili, tabia na historia ya
ulipaji wa madeni kwa mkopaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
wakati wa kutangaza kupatikana Ripoti za Taarifa ya Mikopo (CIRs) pamoja
na maelezo kwa watumiaji wake kwa lugha ya Kiswahili, Meneja wa Dun
& Bradstreet Tanzania, Junaid Malik alisema, ‘Kwa leo ni hatua kubwa
na muhimu kwetu kwa kuweza kutoa ripoti hizi kwa lugha ya Kiswahili.
Hii inathibitisha dhamira yetu ya kuendelea kuwahudumia wateja wetu kwa
huduma bora zaidi. Hatua hii itafanya ripoti hizi kueleweka vizuri na
zaidi na zitawafanya wakopeshaji pamoja na wakopaji kuzitumia kwa ubora
zaidi’.
Malik aliongeza kuwa
lugha ya Kiswahili ndio lugha mama kwa Watanzania. Kupatika kwa ripoti
pamoja na taarifa hizi kwa lugha hiyo zitaongeza uelewa zaidi na
kuwafanya wakopaji kusimamia mikopo yao na kuwa na nidhamu nzuri ya
ukopaji wa fedha.
Malik alisema, ‘Wakati Ripoti zetu za Taarifa
ya Mikopo zikiendelea kuwa kuwa rahisi kwa kuelewa na upatikanaji wake,
bado zinaendelea kubaki kuwa muhimu sana kwenye kufanya maamuzi. Taarifa
na ripoti hizi zinajumuisha maelezo ya mkopaji pamoja na alama za
kulipa mkopo, viashiria vya uwezekano wa kulipa mkopo pamoja na taarifa
za mikopo inayopatikana kutoka makampuni ya mitandao ya simu za mkononi.
Taarifa hizi pia hutoa maelezo ya mkopo wa mtu binafsi na uwezekano wa
kurejesha hata pale hali inapokuwa tofauti na matarajio. Vile vile,
taarifa ya mikopo ina alama ya mkopo iliyotengenezwa kwa ubashiri na kwa
kuzingatia hali na mazingira ya mfumo wa fedha wa Tanzania.
Dun
& Bradstreet Credit Bureau Tanzania inasimamiwa na Benki Kuu ya
Tanzania chini ya kanuni za 2012 (CREDIT REFERENCE BUREAU)
No comments:
Post a Comment