Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa
ziara iliyofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi za
Ulaya na Falme za nchi za Kiarabu hivi karibuni zimeiwezesha Tanzania
kusaini mikataba 42 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 19.
Dkt.
Nchemba ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwa njia
ya mtandao wa zoom na matangazo yake kurushwa moja kwa moja na mitandao
mbalimbali ya kijamii wakati akifafanua manufaa yaliyopatikana katika
ziara hizo zilizofanyika katika nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Falme za
Nchi za Kiarabu.
Dkt. Nchemba alifafanua kuwa akiwa nchini
Ufaransa na Ubelgiji, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alishuhudia
utiwaji saini wa mikataba sita yenye thamani ya shilingi za Tanzania
trilioni 1.77 na miradi mingine 36 yenye thamani ya shilingi trilioni
17.35 za Tanzania, iliyosainiwa Dubai, katika nchi za Falme za Kiarabu.
Alisema
kuwa mikataba hiyo inahusisha miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo
ujenzi wa awamu ya tano wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar
es Salaam (Euro milioni 178), sekta ya kilimo kupitia Benki ya Kilimo
(Euro milioni 81), na msaada wa Euro milioni 425 kutoka Kamisheni ya
Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt.
Nchemba alifafanua kuwa hati za makubaliano 36 zilizosainiwa Dubai
wakati wa mkutano wa biashara na uwekezaji, zinahusisha hati 12
zilizosainiwa kati ya Wizara na Taasisi za Serikali na wawekezaji
mbalimbali katika sekta za umma na binafsi na hati nyingine 23 zilitiwa
saini kati ya kampuni binafsi za Tanzania na kampuni binafsi za nje.
Alisema
kuwa miradi itakayotekelezwa kutokana na fedha hizo ambazo ni mikopo
yenye masharti nafuu na misaada itazalisha ajira zipatazo 200,000 katika
kipindi cha miaka minne ijayo itakuwa na manufaa mengi ikiwemo kuongeza
wigo wa kodi ya Serikali na kuboresha maisha ya wananchi.
Mjadala
huo uliwashirikisha pia baadhi ya mawaziri, akiwemo Waziri wa Viwanda
na Biashara Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nishati Mheshimiwa
Januari Makamba na Wakuu wengine wa Taasisi za Umma walionufaika moja
kwa moja na mikataba iliyosainiwa kutoka pande zote mbili za Muungano,
Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 5, 2022
MWIGULU AANIKA MANUFAA YA ZIARA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UGHAIBUNI
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment