A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 15, 2022

Wasafi Wampa Dkt. Abbasi Keki Ya Birthday, Usiku Wa Wapendanao

 Na. John Mapepele



Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amepamba hafla ya  Usiku wa Mahaba  ndi ndi ndi  baada ya kuandaliwa keki maalum ya siku yake ya kuzaliwa na kuimbiwa wimbo wa kuzaliwa ulioongozwa na Diamond Platnumz.

Dkt. Abbasi alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa waliokuja kushiriki kwenye hafla hiyo tarehe 14 Februari 2022 ambayo ni siku ya wapendanao (Valentine) na ghafla mshereheshaji wa hafla hiyo  Zembwela kutangaza kuwa wasafi wameandaa keki maalum kwa Dkt Abbasi.
 
Kwa upande wake Dkt. Abbasi aliishukuru Wasafi kwa kitendo hicho cha kumpa keki na kumwimbia wimbo wa kuzaliwa.

" Ndugu zangu niseme  wazi kuwa sikutegemea wala kuwaza hii surprise, ninawashukuru sana, kitendo mlichonifanyia hakiwezi kunitoka kwenye kumbukumbu za maisha yangu." Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Katika hafla hiyo wasanii mbalimbali walitumbuiza  huku msanii maalum wa siku Zuchu  akikonga  nyoyo za washabiki  huku mamake bi Hadija Kopa na Bosi wake Diamond Platinum wakiimba pamoja kwenye baadhi ya nyimbo na kushangiliwa na umati wa washabiki.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanasiasa na watu mashuhuri.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages