Wakazi wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia
mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi
(residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya
sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo.
Wanamshutumu mfanyabiashara huyo Bw. Shayo kwa kuvunja
sheria za matumizi ya ardhi kwa ukumbi
wa sherehe na bar kubwa kwenye la eneo
ambalo limepimwa na mamlaka za Serikali kwa ajili ya makazi, na sio biashara.
"Tunashindwa kulala usiku, watoto wetu wanashindwa
kujisomea usiku kwa kelele na ghasia zinasababishwa na ukumbi huu,"
amesema bw.Mika Moza, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
"Serikali imetumia fedha nyingi za walipa kodi kupima
maeneo haya ya makazi, iweje leo mtu anabadilisha matumizi ya ardhi kiholela
kwa kufanya biashara kama hii yenye athari kubwa kwa mazingira kwa njia ya
sauti/ kelele, alafu serikali ya mtaa iko kimya," amesema mkazi mwingine,
Kulwa Muga
Wakazi wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko yao (kwa
maandishi) kwa Afisa mipango miji- Manispaa ya Temeke tangu Mwaka 2013, lakini
mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
"Mfanyabiashara huyu Bw. Shayo, ni mbabe na kwa sababu
ana pesa kiongozi wa serikali ya mtaa, maafisa wa mipango miji -Temeke
Manispaa, wote wametiwa mfukoni, hawawezi kuthibiti jambo hili, hali
inayosababisha hadha kubwa kwa wakaxi wa eneo hili," Bi. Moza Mrope,
amadai mkazi mwingine.
Kuthibisha mahusiana wenye mashaka kati mfanyabiashara huyo,
wakazi wanasema baada ya kuvunja sheria kwa miaka za ya tisa, hivi karibuni
maafisa mipango miji -Temeke manispaa wamemshauri Bw. Shayo, kubadilisha
matumizi ya kiwanja hicho No. 686, Kitalu E, kutoka makazi kwenda biashara,
jambo ambalo ni "uvunjifu wa sheria za mazingira."
"Kumruhudu abadilishe matumizi ya kiwanja -kutoka
makazi kwenda biashara, ni kosa kwa sababu maeneo haya yamepimwa kwa ajili
makazi, na si biashara...Manispaa wakiruhusu jambo hili watakuwa wamebariki
rasmi uchafuzi wa mazingira na uvunjaji wa sheri za mazingira, bila kujali
athari za kelele na uchafu huu mkubwa wananchi walio wengi.
Alipohojiwa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Bw.
Omary Katoto amesema "Sio wakazi wote wanalalamika kuhusu jambo hili,
ninachofahamu mimi ni kwamba kulikuwa ugomvi kati ya mfanyabiashara huyo na mtu
mmoja katika eneo hilo."
"Miaka kama mitatu iliyopita walipelekana polisi,
walitishiana maisha sijui, lakini niitwa kama Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa,
nikawasihi polisi watuachie jambo lile tukalisuhishe kirafiki kama wa mtaa
mmoja, walikubali ...tulikaa chini tuongea na pande zote mbili, tukamaliza. Leo
hii nashangaa kuone jambo hili nimeibuka tena.".
Alipotafutwa, Afisa Ardhi-Temeke Manispaa, Salumu Ali,
amesema “Njia rahisi kwa wakazi hao ni kupeleka malalamiko yao kwa maandishi
kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili kuweka pingamizi la kuzuia mabadiliko ya
matumizi ya Ardhi ambayo Bw. Shayo, amepanga kuyafanya—kutoka Makazi kwenda
biashara.”
“Kama mamlaka, tutapokea maoni na mapingamizi ya wananchi
hao, na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za maswala ya
Ardhi. Hilo ndo naona kama suluhisho kwa wakazi hao wanaolalamika.”
No comments:
Post a Comment