A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 24, 2022

MELI YA MV MBEYA II KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI

 Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imesema Meli ya MV Mbeya II itaanza kufanya kazi ya kusafirisha abiria na Mizigo hivi karibuni ikiwa ni baada ya kupata dhoruba ya Upepo na Mawimbi Mei, 2021.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka wakati akifafanua juu ya usafiri wa Meli katika ziwa Nyasa kwa waandishi wa habari leo Februari 23, 2022 jijini Dar es Salaam. Amesema Meli hiyo imekatiwa Bima na taratibu za kiofisi zinaendelea ili kuweza kupatikana kwa fedha za Bima kwaajili ya kununua mtambo (Main Engine) mpya kwaajili ya kuwekwa ili iweze kuanza kazi tena.

Amesema kuwa mapema Meli hiyo ilipigwa na dhoruba na ikasababisha kuharibika hivyo ikalazimu kuipandisha chelezo kwa matengenezo.

Amesema kuwa matengenezo hayo yalikamilika na Meli ikapata vibali vyote vya kuendelea na kazi ilipofika Januari 27, 2022 lakini Mapema Februari 2022 Meli hiyo ikiwa kwenye safari zake za kawaida ikapata hitilafu kwenye mtambo wake mmoja wa kuendeshea ambapo iliharibika Mkono wa Piston moja.

Mhandisi Mattaka amesema kuwa utafiti umeonesha kuwa tatizo hilo lilitokana na 'Material Failure' na sio mapungufu ya kiuendeshaji.

Serikali kupitia TPA inaendelea kupunguza tatizo la Usafiri wa abiria na uchukuzi kwenye ziwa Nyasa ikijenga vyombo vya usafiri majini vitatu ambapo meli ya mizigo ilijengwa kwa Shilingi Bilioni 5.5 na meli ya abiria na mizigo ilijengwa kwa shilingi Bilioni 9.
Naibu Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 23, 2022 wakati akifafanua juu ya Usafiri wa meli zilizopo katika Ziwa Nyasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages