Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa
Habari Jijini Dar es Salaaam leo Oktoba 17, 2021jinsi
itakavyotumia Shilingi bilioni 90.2 za mgao wa mkopo wa Shirika la
Fedha Duniani (IMF) katika maeneo makuu matano ambayo yameathirika zaidi
kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itazitumia Shilingi bilioni 90.2 za mgao wa mkopo wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) katika maeneo makuu matano ambayo yameathirika zaidi kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19 ikiwemo kukarabati na kujenga miundombinu ya utalii katika maeneo ya hifadhi za Taifa ili kuongeza watalii wanaoitembelea Tanzania.
Hatua
hiyo imekuja kufuatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupata mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi Trilioni 1.3. kutoka
Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya Kampeni ya Maendeleo kwa
Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambao umeelekezwa kwenye
baadhi ya Wizara zikiwemo TAMISEMI, Afya, Elimu na Wizara ya Maliasili
na Utalii.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameyasema hayo wakati
akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaaam leo Oktoba 17,
2021. Amesema eneo la kwanza litakuwa ni Kuziwezesha Taasisi za Wizara
zilizoathirika zaidi kutokana mlipuko wa UVIKO-19 ambazo ni TANAPA,
TAWA, NCAA, TFS na Makumbusho ya Taifa ziweze kutekeleza majukumu
ipasavyo kwa kuziwezesha kuboresha miundombinu na kununua vifaa
mbalimbali.
“Kupitia
fedha hizi tutajenga na kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa
4,881, barabara hizi zitachochea shughuli za utalii ambazo zimetetereka
na kuwezesha watalii kuingia katika hifadhi zetu, janga la Uviko-19
lilisabaisha kupungua kwa watalii na mapato yatokanayo na utalii kiasi
cha kuzifanya taasisi za uhifadhi zishindwe kujiendesha na miundombinu
kuharibika,” amesema Dk Ndumbaro.
Amesema
uboreshaji huo wa miundombinu utafanyika katika hifadhi za Taifa za
Serengeti, Mkomazi, Katavi,Tarangire, Nyerere, Kilimanjaro, Saadani,
Gombe, Ngorongoro pamoja na maeneo ya Misitu Asilia 10 inayosimamiwa na
Wakala wa Huduma za Misitu -TFS.
Dkt.
Ndumbaro ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika katika ununuzi wa mifumo
ya kielektroniki kufanya ufuatiliaji katika taasisi mbalimbali, mitambo
ya ujenzi, kukarabati na kujenga viwanja vya ndege nane ndani ya hifadhi
za Taifa ikiwemo Serengeti na kujenga malango matano katika baadhi ya
hifadhi.
Sambamba
na hilo wizara hiyo inaenda kuboresha na kudhibiti ubora wa huduma za
utalii ambazo zimeshuka wakati wa Uviko-19 ikiwemo hoteli, kutoa mafunzo
na kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato katika vituo vya utalii.
Kwa
mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, idadi ya watalii imeongezeka
mwaka huu na inaweza kuvuka matarajio ya awali yaliyowekwa. Kati ya
Januari hadi Septemba 30 mwaka huu, Tanzania imepokea watalii wa
kimataifa 623,800.
Idadi
hiyo iko juu ikilinganishwa na watalii 620,000 walioingia Tanzania kati
ya Januari na Desemba mwaka jana. Dkt. Ndumbaro amesema Wizara
itaimarisha masoko na kutangaza utalii ambapo kwa kukarabati vituo saba
vya urithi wa kiutamaduni na kununua vifaa kwa ajili ya kutolea taarifa
za utalii kwa njia ya kidijitali
Tunafahamu
“Royal Tour” ameianzisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan akaifikisha mahali, sisi hatutaki ipoe, tunakwenda
kutanua wigo wa “Royal Tour” kutangaza zaidi vivutio na maeneo
mbalimbali” amesema Dk Ndumbaro.
Pia Wizara itashiriki na kuwezesha maonesho makubwa mawili ya utalii ya kimataifa ili kutangaza zaidi vivutio vya utalii.
“Eneo
tatu tunakwenda kuimarisha mazingira ya biashara ya utalii kwa
kuhakikisha kwamba usalama na huduma za afya katika vituo vya utalii
zinakuwa katika kiwango cha kimataifa,” amesema waziri huyo.
No comments:
Post a Comment