Na Mwandishi Wetu
Afisa
Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Jafarani Mapua
ameipongeza Menejimenti ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
kuona umuhimu wa kufanya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha mabinti wa
Wilaya hiyo kupenda masomo ya sayansi kwani ni heshima ya pekee kwao.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mapua amesema kampeni hiyo imelenga
kuhamasisha na kishawishi wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi na
kuongeza udahili wa wanawake wanaosoma masomo hayo ambao kwa muda mrefu
umekuwa chini sana.
Aidha,
amesema kwa kampeni hiyo inayotarajia kufanyika mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Njombe, Mbeya na Iringa kwa kiasi kikubwa utahamasisha na
kubadilisha mtazamo wa wanafunzi wa kike kuona masomo ya Sayansi si kwa
wanafunzi wa kiume pekee.
"Kwa
kuwa sasa Taifa leo linaelekea kwenye uchumi wa viwanda, hivyo tutumie
fursa hii kuwahamasisha mabinti zetu waone fursa zilizopo mbele yao ni
nyingi katika kukuza uchumi wa viwanda, jitihada zenu katika masomo
zitawapa nafasi kubwa katika soko la ajira katika Sayansi, Teknolojia na
uhandisi ambazo ndio chachu kuu ya kufikia Tanzania ya viwanda,"
amesema.
Mapua amesema mabinti wa
wilaya hiyo wamepata bahati kubwa kukutana na wanasayansi wa DIT, ujio
wao una chachu kwao kubadilishana mtazamo juu ya masomo ya Sayansi na
kuyaona kama masomo mengine na kuongeza bidii ili watengeneze
wanasayansi na wahandisi wengi wanawake.
"Naishukuru
kwa mara nyingine DIT kwa kuona umuhimu wa wilaya yetu, kuzindua
kampeni hizi, jitihada zenu si bure zitasaidia kuzalisha wanasayansi
wanawake wengi ambao wataweza kutatua changamoto mbalimbali katika jamii
ya watanzania," amesema Mapua.
Mratibu Jinsi Mradi wa Rafiki DIT Dr Asinta Manyele akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Sekondari Ruangwa
Mhandisi
Mitambo kutoka Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), Anna
Kisioki akitoa uzoefu wake kwa wanafunzi wa kike wa Wilaya ya Ruangwa
No comments:
Post a Comment