Na.Vero Ignatus Arusha
Rais wa jamburi ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza mkuu wa wa mkoa wa Arusha John Mongela kwenda wilaya ya Ngorongoro kuangalia tofati zilizopo Kati ya wananch wanaoishi ndani ya hifadhi na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuangalia namna ya kutatua
Mhe.Rais alisema kuwa huko awali kulikuwa na migogoro mingi Sana, kwani vijiji vingi vimeingia kwenye hifadhi ,lakini wakaangalia migogoro hiyo kwa undani zaidi ya vijiji 100 wameamua kuviacha vilipo, kwani wakivihamisha hakuna pa kuvipeleka
Aidha alimshukuru Leigwanani Kisongo kwa kumwambia kwamba Serikali ikikaa pamoja na wafugaji wanaoishi ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mgogoro huo utatatulika,hivyo Rais wameahidi kumtuma mkuu wa mkoa kutafuta Suluhu.
"Vijiji zaidi ya Mia moja tumeviacha vibakie vilipo ,tukiviahamisha hatuna pa kuvipeleka,Ila nakushukuru Sana Leigwanani Kisongo kwamba umetuambia tukikaa na sisi mgogoro utatatuta,nataka nikuahidi namleta mkuu wa mkoa aje kukaa na ninyi yakimshinda nitaingia mwenyewe" Alisema Rais.
Wakati huohuo Mhe.Rais amempa miezi 3 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya karatu Rajabu Karia Magara kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa hospital hiyo ili kumaliza tatizo la wqgonjwa kukosa huduma ya matubabu
Karatu Kuna hospitali ya wilaya ambayo imeanzwa kujengwa kuanzia mwaka 2019 fedha yote umetolewa ipo pale iqna hospitali haijaisha, nakupa miezi mitatu kwasababu fedha yote unayo sioni kwanini hospital haijaisha Ina mwaka wa pili Sasa haijaisha"Alisema Mhe.Samia
Amemtaka kuhakikisha kuwa hospitali hiyo inamalizika kwa muda alioutoa ili akienda Karatu nikute imemalizika nije niifungie na wannachi wapate huduma
tukiviahamisha hatuna mahali pa kuvipeleka
Akizungumza juu ya ujenzi wa Stendi Jiji la Arusha Mhe.Rais Alisema kuwa hlmshauri Jiji ipeleke mchoro kwani Serikali inamradi wanaandaa wa kuomba fedha hivyo zikipatikana watazileta kwaajili ya ujenzi wa Stendi hiyo
Kuhusu suala la machinga. Alisema kuwa hawawezi kuruhusu sir za mjini kuharibiwa Ila utatafutwa utaratibu Maalum ili kuhakikisha wanpatiwa maeneo ya kufanya biashara zao
Kuhusiana na masuala ya mikopo kwaajili ya kuinua uchumi alisema kuwa mikopo yenye masharti nafuu kwaajili ya manufaa ya Taifa ataiileta Ila mikopo kichefuchefu hatoweza kunichukua kwasababu inawasogeza watanzania inaleta Maendeleo hivyo hataogopa kuichukua
“Nataka kuwaahidi watanzania nitaangalia mikopo yenye unafuu kwa nchi yetu, inayoleta faida kwa nchi yetu hiyo nitaichukua, mikopo chechefu sitaichukua lakini ile ambayo inaleta nafuu kwa nchi yetu, inatusogeza watanzania inaleta maendeleo hiyo sitaogopa nitaichukua,”- Rais Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment