A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 14, 2021

YANGA YAAHIDI MAKUBWA MECHI YA MARUDIANO

 

Na: Stella Kessy 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa Kwa sasa kikosi  kipo tayari Kwa mchezo wa  marudio dhidi ya Rivers United unaoatajiwa kuchezwa Nigeria, Septemba 19.

Kikosi hicho ambacho kinayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilipoteza mchezo wa awali walipoteza nyumbani Kwa  0-1 Rivers, United.

Mchezo wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kwa kuwa kila timu inasaka ushindi.

Akizungumza katika kipindi cha michezo Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa Yanga bado ina nafasi ya kufanya vyema katika mchezo huo wa marudiano huku  akiwaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwa bega kwa bega.

Aliongeza kuwa licha ya kuwa watakuwa ugenini lakini wana nafasi kubwa ya kupata ushindi Katika mechi ya marudiana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages