A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 8, 2021

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA,MMOJA AJERUHIWA BAADA YA FUSO KUGONGANA USO KWA USO

 Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha


KAMANDA  wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo CP JUSTINE MASEJO amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu watano huku mmoja akijeruhiwa.

Akizungumza kuhusu ajali hiyo Kamanda Masejo amesema  leo Septemba 8,2021,muda wa saa 10 Alfajiri katika Barabara ya Arusha/Moshi  konoike kijiji cha Kolila Tarafa ya king’ori wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha kulitokea ajali iliyosababisha vifo vya watu watano na majeruhi mmoja.

Kamanda Masejo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso ambapo gari lenye namba za usajili T111 CUU aina ya Mitsubish Fuso lililokuwa linaendeshwa na Herel Lyimo (42) mkazi wa  Holili mkoani Kilimanjaro liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T 612 BNN aina ya Mitsubish Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Peter Mmasi ETER ambaye bado umri wake na makazi yake hayajafahamika.

Amesema  uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari aina ya Mitsubishi Fuso iliyokuwa inatokea Moshi kuelekea Arusha ambapo ilihama upande wa pili wa Barabara na kugongana na gari aina ya Mitsubish Canter lililokuwa linatokea Arusha kuelekea Moshi.

 Aidha baada ya magari hayo kugongana gari aina Mitsubish Fuso lilipitiliza na kuanguka kwenye mtaro uliopo pembezoni mwa barabara.Amewataja waliofariki katika ajali hiyo ni Peter Mmasi ambae ni dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter, Victor Kileo, Vivian Urio na Isack Tembambao walikuwa abiria wa gari aina Mitsubish Canter na ni wakazi wa Baraa jijini Arusha.

Ameongeza katika gari aina ya Mitsubish Fuso aliyefariki ni utingo wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina moja la IDD mkazi wa Himo mkoani Kilimanjaro.Amesema majeruhi katika ajali hiyo ni Heriel Jinja Lyimo ambaye amepelekwa Hospitali ya KCMC nkoani Kilimanjaro kwa matibabu zaidi na miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Jijini Arusha.

Kamanda Masejo ametoa mwito kwa madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini na matumizi sahihi ya alama za usalama Barabarani ili kuepusha madhara makubwa kwa binadamu ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai na uharibifu wa  vyombo vya moto wanavyotumia





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages