- Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.
- Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.
- Awapo mbinu ya kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.
- Wamachinga wakiri kuingilia maeneo ya watembea kwa miguu na kuahidi kuhama.
- Aeleza dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam.
Na: James Lyatuu, Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa
Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya
utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.
RC
Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na
kujionea Kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa
miguu.
Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya
Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya September 13 na
kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.
Aidha
RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na
kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana
na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.
Hata hivyo RC
Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji
biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima
watembea miguu haki zao za msingi.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
No comments:
Post a Comment