A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, September 25, 2021

RC MAKALLA: KAMPUNI ZA VINYWAJI MSITOE VIFAA KWA WANAOFANYA BIASHARA KWENYE MAENEO YASIYO RASMI.

 Asema Katika huu mwezi mmoja wa maandalizi ya Kuwapanga Machinga ni vyema Kampuni hizo zikafnya sensa ya wateja.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Kampuni zote zinazozalisha Vinywaji ikiwemo Soda, Juice na Vilevi kusitisha kutoa huduma ya Vinywaji Wala Vifaa Kama Majokofu, Viti na Meza kwa Wafanyabiashara wanaoendesha Biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi.

RC Makalla amesema Miongoni mwa wasiotakiwa kupatiwa huduma ni wale Waliojenga Vibanda juu ya Mitaro na mifereji, Wanaofanya biashara Kwenye njia za watembea kwa miguu, wanaofanya biashara mbele ya Maduka, wanaofanya biashara Kwenye hifadhi ya Barabara na waliojenga Vibanda mbele ya Taasisi za Umma zikiwemo shule.

Aidha RC Makalla amesema inasikitisha kuona mtu anafanya biashara Kwenye maeneo yasiyo rasmi lakini amepatiwa Viti, meza na Majokofu kutoka kwenye makampuni makubwa ya Vinywaji.

Hayo yote yamejiri wakati wa kikao Cha Shirikisho la Wenye Viwanda CTI kilichoketi leo Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuboresha mazingira ya Uwekezaji na biashara.

 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages