A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, September 23, 2021

NEMC YASHIRIKI MAONYESHO YA SIDO KITAIFA MKOANI KIGOMA.

 Na Editha Karlo,Kasulu.


BARAZA la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) wanashiriki maonyesho ya tatu ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma Wilayani Kasulu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho hayo kwenye banda lao Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC),Dkt. Samwel Gwamaka alisema kuwa kuna wajasiliamali wachache wamekuwa wakifanya shughuli zao bila kuangalia athari za mazingira katika shughuli zao wanazofanya.

Alisema NEMC wamekuwa wakitoa elimu ya mazingira kwa wajasiliamali wadogo ili waweze kulinda mazingira wanapokuwa kwenye maeneo yao ya kazi.

"Suala la utunzaji wa mazingira linapaswa kuwa ni suala ya maisha yetu ya kila siku,tupo hapa kwenye maonesho haya ya SIDO kwaajili ya kutoa elimu kwa wajasiliamali juu ya kutunza mazingira ili uwekezaji wao wanaoufanya usiwe na athari yoyote kimazingira"alisema

Naye Meneja wa baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Benjamin Dotto alisema kuwa kwenye banda lao katika kipindi chote cha maonyesho watakuwa wakiwapatia wajasiliamali elimu ya utunzaji wa mazingira.

"Wajasiriamali wote waliopo hapa kwenye haya maonyesho pamoja na wananchi wafike kwenye banda letu hapa wapate elimu ya utunzaji na kuhifadhi mazingira.

Mfanyabiashara Antony Bulindu kutoka Mkoa wa Tabora amelishukuru Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kwa elimu wanayowapatia juu ya kutunza mazingira katika biashara zao,pia ameishukuru SIDO kwa kuandaa maonyesho hayo ambayo yamewakutanisha wajasilimali na wadau mbalimbali wa sekta ya ukuzaji wa biashara ndogondogo.

Maonesho hayo yameanza tarehe 22 Octoba mwaka huu na kufunguliwa na Makamu wa Rais Dk Philipo Isdor Mpango ambapo yatahitimishwa tarehe 30 mwezi huu


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipo Isdor Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya tatu ya shirika la mkuhudumia viwanda vidogo(SIDO)ambayo kitaifa yanafanyika katika uwanja wa umoja,Wilayani kasulu Mkoani Kigoma (wa tatu kulia) ni Waziri wa Viwanda na Biashara (Mb) Kitila Mkumbo pamoja na viongozi mbalimbali kutoka serikali na uongozi wa Sido
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages