A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, September 12, 2021

KALIMA AHIMIZA USIMAMIZI MAKINI WA MIRADI YA JUMUIYA YA WAZAZI

 

Na.Elisa Shunda, Geita | KATIBU mkuu wa umoja wa wazazi Tanzania jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu, Gilbert Kalima, amewahimiza viongozi na watendaji wa jumuiya wazazi wa CCM kuwa makini katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya jumuiya hiyo.

Kauli hiyo ameitoa mkoani Geita, jana alipotembelea na kukagua mgodi wa Lwamgasa unaoendeshwa na jumuiya ya wazazi mkoa wa Geita.

Amezihimiza kamati mbalimbali zinazosimamia miradi ya kiuchumi kuhakikisha zinazingatia kanuni za fedha na mali za chama na jumuiya zake.

Aidha Ndugu.Kalima amesisitiza kamati ya utekelezaji ya wazazi mkoa wa Geita ihakikishe inafanyia kazi mapungufu mbalimbali yanayoukabili mgodi huo ili uwe na manufaa zaidi katika jumuiya ya wazazi.

Kabla ya kutembelea mradi huo, Katibu mkuu wa wazazi, Ndugu, Kalima, alipata fursa ya kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa na kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi na wanachama kutoa pongezi kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Geita kwa kuhakikisha chama hicho kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kupata ushindi wa 83% na kushika nafasi ya tano kitaifa.

Aidha alitoa wito kwa chama na jumuiya ngazi zote kuanza maandalizi kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa chama na jumuiya zake unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao 2022.

Katika ziara hiyo katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi, Ndugu, Kalima amefuatana na mwanasheria wa jumuiya ya wazazi, ndugu, Beatus Mafuru na Mkuu wa kitengo cha Milki makao makuu ya chama hicho, Ndugu, William Obimbo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages