Afisa wa Kimataifa wa Bidhaa za DRM Steve Hoffman (kushoto),
na Mkurugenzi Mtendaji wa Tristar Group Eugene
Mayne, wakitia saini makubaliano ya BBDA kutoka maili mbali yenye lengo la kufanya
kazi pamoja na kutengeneza na kusambaza na kuuza mafuta ya vilainishi ya
CaltexTM katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Chevron Brands International yaingia Mkataba na Tristar (AFAL) kwenye
leseni ya vilainishi na makubaliano ya utenegenezaji katika Afrika Mashariki.
Mkataba mpya utaimarisha vilainishi vya
Caltex kuongezeka Afrika Mashariki
(Dar es Salaam, Tanzania) Septemba 15, 2021: Kampuni ya Chevron Brands International LLC (Chevron) na AFAL
Manufacturing Limited (AML) iliyopo chini ya Tristar Group, wameingia
makubaliano ya muda mrefu ya kutengeneza na kusambaza na kuuza mafuta ya
vilainishi ya CaltexTM
katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC). Pamoja na kuingia kwenye mkataba huu, Chevron
imeimarisha uwepo wake ambao tayari unakua katika Ukanda wa Afrika Mashariki na
kukabidhi leseni ya shughuli zake kwa AML.
Vilainishi vya mafuta vya chapa ya
Caltex, vimekuwa vikipatikana katika nchi za Afrika Mashariki tangu mwaka 2013
vikisambazwa na kwa makubaliano na Africa Fuels & Lubricants Ltd (AFAL), pia
ya Tristar Group. Kuaminiana na kuridhika kutoka kwa ushirikiano huu
uliofanikiwa, ilikuwa ni sababu kubwa katika utambuzi wa kuingia makubaliano ya
leseni ya muda mrefu. Kwenye upeo huu mpya, Chevron itatoa teknolojia
inayoongoza ulimwenguni, na AML itachanganya, kuuza, na kusambaza vilainishi
vyenye nembo ya Caltex kupitia mtandao wake mpana na kuingia katika soko la
ushindani Afrika Mashariki.
“Chevron ina historia Afrika Mashariki, na tumejipanga katika miongo saba na tulianza ushirikiano na AFAL tangu mwaka 2013. Zaidi ya miaka nane, uhusiano wetu na AFAL umekuwa kwa namna moja hadi nyingine, na tunafurahia kuanza makubaliano mapya na AML, ambayo yatasaidia bidhaa za Caltex kusambaa maeneo yote ya Afrika Mashariki. Makubaliano haya yatajumuisha kukua na kusambaa kwa bidhaa hizo,” alisema Douglas Rankine, Meneja Mkuu wa Mafuta na Vilainishi Mashariki ya Kati na Afrika. “Pande zote mbili zilijitahidi wakati wa janga la korona na kuafikia mkataba huu, hivyo kuonyesha uhusiano ulioboreshwa unaotegemea uaminifu, uadilifu na utendaji.”
Kufanikiwa kwa makubaliano haya ya leseni na kuongezeka kwa mahitaji ya vilainishi katika mikoa, kulikuwa na sababu kuu katika kujenga zaidi uhusiano kati ya Tristar Group na Chevron, na itatambua kuingia katika soko jipya la Tanzania kama soko la AML.Uhusiano huu wa kimkakati wa muda mrefu ni kielelezo cha kujitolea na uhakikisho wa Chevron kwa wateja, katika masoko ya Afrika Mashariki kutoa bidhaa bora na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya eneo hilo kupitia ushirikiano wa Chevron na AML katika soko la vilainishi vya Afrika Mashariki.
AML ina uhakika kuwa hatua hii
itawezesha chapa ya Caltex kupata sehemu kubwa ya soko katika eneo la Afrika
Mashariki kwa kutumia faida za gharama na ushirikiano wa mchanganyiko wa ndani.
“Kuchaguliwa na Chevron kwa jukumu
hili muhimu ni onyesho la kujiamini katika uhusiano wa muda mrefu kati ya
Chevron na Tristar Group tangu AFAL ilipopewa makubaliano ya usambazaji wa
vilainishi na Chevron mwaka 2013, na itatumika kama sehemu ya uzinduzi wa
vilainishi vyenye asili ya Caltex kupanua mauzo katika ukanda wa Afrika
Mashariki. Tuna hakika kuwa uchanganyaji wa ndani ni hatua inayofaa kwa
biashara hii kubaki kuwa na ushindani, na hatutaokoa juhudi yoyote kuimarisha
msimamo wa chapa ya Caltex Afrika Mashariki,” alisema Mtendaji Mkuu wa Tristar
Group, Eugene Mayne.
Tristar ni Kampuni ya Biashara ya
Kimataifa ambapo Makao Makuu yake ni Dubai, ambayo inatoa suluhisho na vifaa
vya mafuta kwa wateja pamoja na kampuni za kitaifa na kimataifa, na mashirika
ya serikali. Pia inajumuisha vifaa vya nishati katika usafirishaji wa nchi kavu
na majini, maghala maalum, mashamba ya mafuta, biashara ya mafuta ya ndege na
shughuli za usambazaji wa mafuta.
AML imejitolea kutengeneza
vilainishi vya hali ya juu kulingana na viwango vya Chevron na imejitolea
kushughulikia mahitaji ya wateja na matarajio ya soko yanayozidi kuongezeka
nchi za Afrika Mashariki.
Pamoja na uhusiano huu wa
kimkakati, Chevron na Tristar Group, wanawekeza zaidi kufikia kuongezeka kwa mahitaji
ya vilainishi vyenye asili ya Caltex, ambayo inashughulikia sekta ya watumiaji,
biashara na viwanda katika eneo lote la Afrika Mashariki.
-Mwisho -
Kwa mawasiliano Zaidi, tafadhali ongea na:
Christine Wathoni - Mobile: 0722
268 245
E-mail: publicity@pinkafricamarketing.com
Editor’s Notes:
AFAL Manufacturing Limited (AML) is
the license holder for manufacturing Caltex Lubricants in East Africa and will
blend, distribute and sell Caltex lubricants in Kenya, Uganda, Tanzania,
Rwanda, Burundi and Democratic Republic of Congo. AML is a subsidiary of the
Tristar Group which is headquartered in Dubai, UAE. Tristar is a global
business which offers end-to-end fuel logistics solutions to blue-chip clients
including international and national oil companies and intergovernmental
organizations. Its integrated energy logistics platform spans road and maritime
transportation, specialized warehousing, fuel farms, commercial aviation
refueling and fuel supply operations. More information about Tristar is
available at www.tristar-group.co
Chevron
Chevron is one of the world’s leading
integrated energy companies. We believe affordable, reliable and ever-cleaner
energy is essential to achieving a more prosperous and sustainable world.
Chevron produces crude oil and natural gas; manufactures transportation fuels,
lubricants, petrochemicals and additives; and develops technologies that
enhance our business and the industry. To advance a lower-carbon future, we are
focused on cost efficiently lowering our carbon intensity, increasing
renewables and offsets in support of our business, and investing in low-carbon
technologies that enable commercial solutions. More information about Chevron
is available at www.chevron.com.
No comments:
Post a Comment