A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 26, 2021

TAASISI YA WAJIBU YAANDAA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UWAZI NA UWAJIBIKAJI UTAKAOFANYIKA NOVEMBA MWAKA HUU

 TAASISI ya Wajibu imeandaa mkutano wa wadau wa fani tofauti tofauti ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo uwazi wa kifedha na uwajibikaji kama nyenzo kwa nchi za Afrika kufikia maendeleo endelevu ya ushindani katika uchumi wa dunia. 

Akizungumzia mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh amesema kwamba wanatarajia mkutano huo utahusisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali zikiwemo taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo, wanadiplomasia, wanaazaki, wabobezi wa masuala ya uwazi na uwajibikaji, wanataaluma mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema mada nyingine ambazo zitatolewa ni uhuru wa ofisi za ukaguzi za nchi na athari zake kwenye uwazi na uwajibikaji katika mabadiliko kwenye kanuni na mazoea ya ufanyaji ukaguzi wa ndani na nje.

" Je! Serikali za Afrika zina uwazi na uwajibikaji wa kutosha katika kushughulikia janga la covid – 19?Ufanisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuimarisha Uwazi na uwajibikaji wa Fedha na Rasilimali za Umma barani Afrika," Amesema Utouh.

Amesema kuwa itatolewa pia mada ya kuwa wazi zaidi na kuwajibika na mipango ya Ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika sekta ya uziduaji barani Afrika.

Utouh amesema uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi wa Serikali zote duniani una umuhimu wa kipekee katika kuletea wananchi maendeleo.

" Ninatoa rai kwa wadau wote wa uwazi na uwajibikaji kutoka ndani na nje ya nchi kuweza kushiriki Mkutano huu wa Kimataifa wa ITAC 2021 ambao ni fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo ya nini kifanyike ili kukuza na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa maendeleo ya nchi za Afrika.

Tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 500 wa mkutano huo. Vilevile, wanatarajia kuwa na Mgeni rasmi ambaye ni mmoja wa viongozi wakubwa kitaifa nchini, ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu hatuwezi kumtaja hivi sasa," Amesema Utouh.

Mkutano huo unatarajia kufanyika Novemba 18-19 mwaka huu katika Hotel ya Mount Meru iliyopo jijini Arusha.

Kwa habari na Maelezo zaidi bofya https://www.wajibu.or.tz/


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh akizungumza mbele ya Wadau  kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji ( International Transparency and Accountability Conference – ITAC) unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba, 2021 katika Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha, Tanzania.Amesema  mkutano  huo utawahusu Wadau wa fani tofauti tofauti ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo uwazi wa kifedha na uwajibikaji kama nyenzo kwa nchi za Afrika kufikia maendeleo endelevu ya ushindani katika uchumi wa dunia. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh (wa pilia kushoto) akiwa na baadhi ya  Wadau  wengine wakati wa uzinduzi wa  maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji ( International Transparency and Accountability Conference – ITAC) unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba, 2021 katika Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha, Tanzania

 wakati wa uzinduzi wa  maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji ( International Transparency and Accountability Conference – ITAC),pia kulikuwepo na majadilialiano ya mada kutoka kwa Wadau  zilizohusu mambo ya uwazi na uwajibikaji

Meneja wa Utafiti na Miradi kutoka Taasisi ya WAJIBU, Moses Kimaro akiwakaribisha Wadau mbalimbali waliofika kushiriki maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji ( International Transparency and Accountability Conference – ITAC) unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba, 2021 katika Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha, Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh (katikati) akiwa na baadhi ya  Wadau  wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zikijadiliwa mara baada ya uzinduzi wa  maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji ( International Transparency and Accountability Conference – ITAC) unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba, 2021 katika Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha, Tanzania.

Baadhi ya Wafanyakazi wa taasi ya WAJIBU wakijadiliana jambo kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye kutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages