Ni sehemu mkakati
wake wa kuwafikishia wananchi msaada wa kisheria kwenye maeneo yao.
Awaalika Wenye
Migogoro kuwasilisha kero zao.
Asema kila mmoja atapata haki yake kwa mujibu wa Sheria.
Awaandaa wataalamu wa
sekta mbalimbali kwaajili ya kuhudumia kila atakaefika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla anatarajiwa
kuanza rasmi ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi wa
Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za
Wananchi.
RC Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu ya
August 30 kwenye Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers, August 31 Jimbo
la Kibamba, September 01 Jimbo la Segerea, September 02 Jimbo la Mbagala na
September 03 Jimbo la Kigamboni ambapo zoezi litaanza kuanzia Saa mbili Asubuhi
Hadi majira ya jioni.
Aidha RC Makalla amesema kutakuwa na jopo la Wataalamu wabobezi wakiwemo Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote wanaojihusisha na masuala ya kisheria.
Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi wote
Wenye Migogoro kutumia Fursa hiyo kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze
kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria.
No comments:
Post a Comment