Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Jenga Hub ambae pia ni Miss Tanzania wa zamani Nancy Sumari (kushoto), wakitiliana
saini na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Kids Finance na Tracy zilizoanzishwa
na msichana wa miaka 11, Tracy Rabi, kwaajili ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja
yenye lengo la kuwasaidia watoto wa Kitanzania namna bora yamatumizi ya fedha
na ujasiliamali wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya Mipango Lilian
Makoi, Mwanzilishi wa program ya Natokaje kidigitali Gertrude Mligo, hafla hiyo
imefanyika jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam....................
Taasisi isiyokuwa ya
kiserikali ya Kids Finance na Tracy, zilianzishwa na msichana wa miaka 11,
Tracy Rabi ambaye leo ametia saini mkataba wa makubaliano na Miss Tanzania wa
zamani na mwanzilishi wa Jenga Hub, Nancy Sumari, kwa ajili ya ushirikiano wa kufanya kazi pamoja kwa kuwapa
elimu ya kisasa watoto wa Kitanzania juu ya ujasiriamali nan a matumizi mazuri
ya fedha.
Ushirikiano huo pia
umejumuisha Natokaje Kidigitali, iliyoanzishwa na Getrude Mligo. Natokaje
Kidigitali imekuwa ikijihusisha na watoto wenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 17
kwa kushirikiana na mfanyabiashara aliyepata mafanikio makubwa Mohammed Dewji
na wakongwe kama Gillsant Mlaseko.
Wamekuwa wakiwapa watoto
fursa ya kujifunza kutoka kwa watu wenye vipaji nchini.Nancy alisema kuwa amekuwa
akiendesha taasisi yake kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka
mitatu sasa na kuwasaidia kujifunza masuala mbalimbali ya kibiashara
yanayokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa.
Msichana mwenye umri wa
miaka 11, Tracy Rabi, sio tu anaandika
vitabu vya kifedha na ujasiriamali kwa watoto lakini pia alianzisha Maonyesho
ya Uzoefu wa Ujasiriamali kwa Vijana wa Tanzania ambayo hukusanya pamoja watoto
wenye miradi ya ujasiriamali ili kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa watoto
wengine, kama njia ya watoto ya kujaribu na kujifunza ujuzi wa ujasiriamali
tangu wakiwa na umri mdogo.
Taaisi hizi tatu zimeungana
pamoja ili kutoa fursa ya aina yake kwa watoto wa Tanzania kuongeza nafasi ya
kujifunza ujasiriamali na kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa nchini.
Hii pia inakwenda sambamba
na lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa kizazi kijacho kinapata teknolojia na
vifaa muhimu vya kisasa ili kuendanana na kasi ya teknolojia. Kuboresha
upatikanaji wa teknolojia ni moja ambayo ni ajenda kuu ndani ya sekta ya
mawasiliano haswa, kwa njia ambazo zinafaidisha vizazi vipya.
Kampeni hiyo inayoitwa
Children Bootcamp, imeanzishwa mwaka huu ambapo inatarajia kusaidia watoto
zaidi ya 200 kutoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Ninaamini kwamba sio mapema
kwa vijana kuanza kujifunza kuhusu biashara na fedha kama watoto, tunatumia
zaidi ya miaka 16 shuleni kupata ujuzi wa kutusaidia kupata pesa, ni muhimu
watoto wawezeshwe kupata pesa, kuweka pesa na ujuzi wa kukuza pesa, kuwasaidia
kuepukana na umaskini au mitego ya madeni inayosababishwa na ukosefu wa elimu
ya kifedha,” alisema Tracy Rabi.
“Watoto wanatakiwa kuelewa
hatua za awali za kuhifadhi fedha, thamani ya fedha, kuanzisha biashara na
kujua mbinu za kuendesha biashara ambazo ni hatua muhimu kwa haki za binadamu,”
alisema Rabi
“Tunafurahi pia tutakuwa na
program za watoto na zinazopatikana
Tracy Kids Finance ambaye zinaonyesha kuwa hata watoto wadogo wanaweza kupata
ujuzi na kuwajengea mazingira ya kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Ujuzi
upo wa unapatikana katika ulimwengu tunaoishi kwa njia ya za kidijitali,”
aliongeza.
Nancy Sumari aliongeza
“Tumejipanga kuleta mapinduzi katika kuwajengea uwezo watoto kwenye vitengo
vifuatavyo:
● Elimu ya Fedha
● Elimu ya Kidijitali
● Ujasiriamali
No comments:
Post a Comment