1
UZINDUZI WA POMBE KALI MPYA YA KIWINGUDar es Salaam Jumatano 14 Julai 2021
: Kampuni ya KILIMANJAROBIOCHEM LIMITEDinazindua kinywaji kipya aina ya pombe kali ya KIWINGU.Kinywaji hichi kitazalishwa katikakiwanda chao kilicho katika kijiji cha Kifaru, wilayaya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro nakitasambazwa kuanzia Dar es Salaam na Mwanza. Kinywajihichi kipya kimetengenezwa kwakuzingatia mahitaji ya wanywaji na kwa utaalamu wahali ya juu.Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu waziri wa viwandaMhe. Exaud Kigahe, ambayealikuwa mgeni rasmi alisema kuwa serikali itaeendeleakuunga mkono wawekezaji wa ndanina nje ya nchi ili kufanikisha mikakati wa kuifanyaTanzania kuwa nchi ya Viwanda akiongeana waandishi wa habari na wafanya biashara katikasekta ya usambazaji wa pombe Dar esSalaam “Nawapongeza Kilimanjaro Biochem Limited, kwakuzindua kinywaji chao kipyakiitwacho Kiwingu, kuingia sokoni, sambamba na mikakatiyao ya kuyateka masoko zaidi.Tumejumuika siku ya leo pamoja na wafanya biasharakatika sekta ya usambazaji, na ni isharakwamba mnatambua manufaa ya bidhaa hii mpya katikabiashara zenu na pia mngependakuwa sehemu ya mafanikio na ukuzaji wa uchumi. ”Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa KilimanjaroBiochem, Bw. Mehul Patelalisema “Soko la vinywaji nchini Tanzania lina ushindanimkubwa. Tunajali ubora na kuhakishaviwango katika kila hatua ya utengenezaji wa kinywajichetu kipya kinacho itwa Kiwingu.Katika ubora wetu tunatumia ethanol yenye viwangovya juu isiyo sababisha uchovu baadaya kunywa na yenye kiwango cha juu cha pombe.”Kampuni ya Kilimanjaro Biochem imewekeza takribaniTZS. 11.5 Billioni, kwa ajili yauwezeshaji na uzalishaji wa bidhaa hii mpyaitazoenda kusaidia uchumi kwa kutoa ajira kwawatanzania 200 katika ajira rasmi, na zaidi ya watanzania50 katika ajira zisizo rasmi kamawakulima wadogo na wa kati wanaojishughulisha na kilimocha mtama katika mashambayaliyopo wilayani Mwanga na wilaya za jirani.Kilimanjaro Biochem inashirikiana na jamii inayoizungukakwa kushiriki kuimarisha huduma za jamii na kuchangia kupitia programu ya uwajibikajiwa huduma za kijamii ( CSR ) kwa kutoakiasi zaidi ya 24 Milioni
kila mwaka
kuwekeza kwenyeelimu, afya na maji.Mkuu wa usambazaji na mauzo kutoka Kilimanjaro BiochemEng Herman Mathias aliongezakuwa kinywaji cha Kiwingu kinapatikana kwenye chupandogo yenye ujazo wa mililita 250 nausambazaji wa kiwingu utaanza katika mkoa wa Dar esSalaam na mikoa yote ya kanda yaziwa na akawashukuru mawakala wote waliokuwa wamehudhuriauzinduzi huo.Mkuu wa masoko aliongeza “Wananchi wote wana wezakupata taarifa mbalimbali kuhusuKiwingu na kuzungumza moja kwa moja na wasaidizi kupitiamitandao yao ya kijamii, kupitiaWhatsapp namba 0737 72 7 182 ili kujua zaidi kuhusuKiwingu.
Kuhusu Kilimanjaro Biochem
Kilimanjaro Biochem Ltd iliyo katika kijiji cha Kifaruwilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro niKampuni ya Uwekezaji wa Kigeni ya 100% iliyoanzishwamnamo 2008.Kilimanjaro Biochem ltd hutengeneza bidhaa za ExtraNeutral Alcohol (96.4%) na liquid LCO2(99.99+% purity) ambazo hutumika katika viwanda vyavinywaji na pombe na ambayohutumiwa katika tasnia ya Medical Spirit na Hand Sanitizer.Ni kampuni ya kwanza ya utengenezaji wa kemikali yaBIO-Chemicals nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment