Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa
habari katika Uzinduzi wa tela maalumu kwaajili ya kubebea mazao kwa
mkulima. Uzinduzi umefanyika katika banda la NDC katika Maonesho ya 45
ya Kimataifa ya Biashara yabayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la maendeleo (NDC), Rhobi Sattima akizungumza na waandishi wa habari katika Uzinduzi wa tela maalumu kwaajili ya kubebea mazao kwa mkulima. Uzinduzi huo mefanyika katika banda la NDC katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yabayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amelipongeza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kushirikiana na TEMDO pamoja na CARMATEC kwa kutengeneza Tela litakalosaidia wakulima wakulima kusafirisha mazao na pembejeo katika sekta ya kilimo.
Tela hilo limetengenezwa na kiwanda cha KMTC ambacho husimamiwa na NDC.
Profesa Mkumbo ameyasema hao leo Julia 7,2021 wakati akizindua Tela hilo katika Maonesho ya 45 ya biashara ya Kimataifa ya yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema Mazao mengi ya wakulima yamekuwa yakiaribika njiani kabla ya kufika sokoni kutokana na changamoto ya usafiri hivyo Tela hilo linaenda kuwa tiba bora kwa wakulima na litawapunguzia gharama za kusafirisha mizigo na bidhaa.
"Tela hili limetengenezwa hapa hapa Tanzania , ambapo kiwanda chetu cha KMTC kipo, hii inaonesha kwamba viwanda vyetu kwakweli vinaweza kutengeneza bidhaa za msingi na moja ya malengo yetu ni kukidhi mahitaji ya soko la ndani ili tuanze kutumia na kula bidhaa ambazo tunazalisha sisi wenyewe hapa". Amesema Prof.Mkumbo.
Nae Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amesema uzinduzi wa tela hilo utaenda kuongeza thamani ya uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo ambapo moja wapo ya changamoto kubwa ni kwenye usafirishaji mazao na bidhaa mbalimbali.
" Bidhaa zinakuwa zinaharibika au kutokufika kwa urahisi katika maeneo husika kwasababu ya kukosa vifaa maalumu na vya bei rahisi kwaajili ya kusafirishia mazao hayo na bidhaa mbalimbali". Amesema Mhe.Kigahe.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la maendeleo (NDC), Bi.Rhobi Sattima amesema kuwa tela hilo lenye uwezo wa kubeba tani tano limebuniwa kwa kuzingatia vigezo vyote vya ubora, ufanisi na usalama wakati linapokuwa linafanya kazi na kuthibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Amesema kuwa tela hilo limetokana na wazo bunifu la kuwa na chombo cha kusafirisha pembejeo na mazao ya kilimo ambalo litakokotwa na trekta linalounganishwa katika kiwanda cha matrekta kilichopo katika eneo la mitaa ya Viwanda TAMCO, Kibaha.
"Tela hili limesafiniwa kwa ushirikiano kati ya NDC,TEMDO na CARMATEC. NDC walitoa wazo bunifu, TEMDO walihusika katika usanifu na michoro na CARMATEC walihusika katika kufanya majaribio ya tela hili". Amesema Bi.Sattima.
Amesema moja ya mchango wa tela hilo kwenye uchumi ni pamoja na mapinduzi kwenye sekta ya kilimo kwani mkulima anaweza kuzalisha bila ya kuwa na changamoto ya usafirishaji wa mazao na pembejeo.
No comments:
Post a Comment