Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko ziarani mkoani Mwanza akikagua miradi ya maendeleo. Katika ziara hiyo Rais Samia amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga
Uzinduzi wa ujenzi wa kipande hicho cha reli ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa kipande hicho cha tano kinachojengwa ndani ya miezi 36 sawa na miaka mitatu.
Kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania kutasaidia kutatua kero ya usafiri kwa kusafirisha mizigo na abiria kwa uharaka zaidi katika nchi za ukanda wa maziwa makuu.
Rais Samia amezindua kipande hicho cha reli kutoka Mwanza hadi Shinyanga chenye urefu wa kilometa 341, ambapo kilometa 219 zitatumika kama njia kuu huku kilomita 122 zitatumika kama njia za kupishana na vituo vya kushuka na kupanda abiria ni 9, huku idadi ya vivuko vya chini vitakavyojengwa ni 44 na vya juu vitakuwa ni 23.
Mapema mwezi Januari mwaka huu, serikali za Tanzania na china zilitiliana saini za makubaliano ya ujenzi wa reli ya kisasa ambao utagharimu jumla ya shilingi za kitanzania trilioni 3.1 sawa na zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.326.
Kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania, kunatajwa kuwa na tija hasa kwa wananchi wa mikoa hiyo kwani zaidi ya ajira elfu 75 zinatajariwa kupatikana kwa miaka yote mitatu ya ujenzi wa reli hiyo.
Kuwekwa kwa jiwe la msingi ni kiashiria cha kuanza kujengwa kwa kipande cha tano, ambapo kipande cha kwanza ni kutoka dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutoporakwenda Tabora, Tabora mpaka Isaka na Isaka hadi jijini Mwanza.
Akizungumza mkoani mwanza baada ya raisi kuzindua awamu ya tano ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka mwanza hadi isaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Michael Zhang alisema kwasasa kampuni hiyo inashirikiana kwa ukaribu zaidi na Shirika la Reli Tanzania TRC kwa kutoa vifaa vya mawasiliano na huduma kwenye miradi ya SGR ikiwemo Mfumo wa wa Teknolojia ya Mawasiliano-Reli (GSM-R) ambayo baadae itabadilika na kuwa mfumo wa LTE-R.
Niimani yetu kwamba chini ya uongozi mpya wa Rais Mama Samia Suluhu, Huawei itaendelea kujenga Miundombinu ya TEHAMA kulingana na Dira ya maemdeleo ya Tanzania 2025" aliahidi
"
No comments:
Post a Comment