Wateja kuwasiliana kwa gharama nafuu na kupata maudhui ya kiislamu kuhusu mfungo wa Ramadhan
Zanzibar, 13 Aprili 2021 - Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, leo imezindua ofa maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake ili kuwawezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu pamoja na kupata maaudhui mbalimbali yenye kuimarisha imani zao katika kipindi chote cha mwezi mtukufu.
Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na kupata taarifa muhimu kama vile nukuu mbalimbali za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala na ujumbe wa sauti utakaowakumbusha nyakati za iftar na nyakati za daku.
Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa alisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha mfungo.
“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii itahakikisha kwamba wateja wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.
Hivi karibuni Zantel ilizindua kampeni yake ijulikanayo kama “Pasua Anga Ki Zantel 4G” kwa lengo lakuwawezesha wateja kujua umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.Katika mwezi huu, waumini wanaweza kutumia mtandao wa 4G kwa kujiongezea maarifa juu ya chimbuko, swala mbalimbali na mambo yakufuata katika kipindi cha mfungo.
“Tunatambua kwamba huduma ya intaneti ni nyenzo muhimu katika kipindi hiki ambapo wengi watahitaji intaneti ili kuangalia vipindi mbalimbali vya dini, kujifunza na kubadilishana taarifa juu ya kipindi hiki cha Ramadhan.Kupitia vifurushi vyetu vya intaneti viliboreshwa wateja wanaweza kufanya mengi zaidi kwa kujiongezea maarifa kupitia mtandao wa 4G na kufanya kipindi hiki kuwa na thamani zaidi kwao,” alisema Mussa.
Naye, Mkuu wa Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi vilivyoboreshwa zaidi vya siku, wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.
“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema.
Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi 2,000 mteja atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata dakika 1,500, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu, jumbe za kuwakumbusha muda wa kufuturu pamoja za kukumbusha muda wa swala.
Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na kuchagua namba 0 ambayo ni ofa ya Ramadhani na atajiunga na kifurushi anachohitaji.
Kuhusu Zantel
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.
Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.
Aidha,Miundombinu hiyo imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali
Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu Zantel tembelea tovuti; www.zantel.co.tz
Rukia Mtingwa – Manager Brand and Communication
Mobile: +255 774 55 9999
r.mtingwa@zantel.co.tz
No comments:
Post a Comment