A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, April 26, 2021

WAZIRI UMMY ATOA SADAKA YA FUTARI KWA TAASISI KUBWA ZA DINI NA VITUO VYA KULEA WATOTO YATIMA JIJINI TANGA

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kulia akimkabidhi msaada wa futari alioutoa Katibu wa Idara ya Taaluma wa Taasisi ya Maawal Islamic Mohamed Shabani ambapo msaada huo wa Futari aliutoa kwa Taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga na Vituo 10 vya Kulea Watoto Yatima na Makazi ya Wazee Mwanzange ili kuwawezesha kuweza kutimiza nguzo muhimu wa uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kulia akimkabidhi msaada wa futari alioutoa Katibu wa Idara ya Taaluma wa Taasisi ya Maawal Islamic Mohamed Shabani ambapo msaada huo wa Futari uliutoa kwa Taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga na Vituo 10 vya Kulea Watoto Yatima na Makazi ya Wazee Mwanzange ili kuwawezesha kuweza kutimiza nguzo muhimu wa uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kulia akimkabidhi msaada wa futari alioutoa kwa Mwalimu wa Taasisi ya Jaamia na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtupie Saidi Juma ambapo msaada huo wa Futari uliutoa kwa Taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga na Vituo 10 vya Kulea Watoto Yatima na Makazi ya Wazee Mwanzange ili kuwawezesha kuweza kutimiza nguzo muhimu wa uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) katika akishiriki kuomba dua na Mwalimu wa Taasisi ya Jaamia na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtupie Saidi Jum mara baada ya kukabidhi msaada huo wa Futari
Sehemu ya watoto yatima wanaolelewa kwenye Taasisi ya Jaamia wakiwa kwenye picha ya pamoja nyumba ya msaada wa vyakula walivyokabidhiwa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho
Sehemu ya msaada uliotolewa
Sehemu ya msaada uliotolewa
Sehemu ya msaada uliotolewa

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ametoa sadaka ya futari kwa taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga na Vituo 10 vya Kulea Watoto Yatima na Makazi ya Wazee Mwanzange ili kuwawezesha kuweza kutimiza nguzo muhimu wa uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 

Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) ametoa msaada huo leo  kwa Taasisi za Tamta,Zaharau,Maawal,Shamsul Maarifa, Rashaad,Nuruhuda Donge,huku vituo vya kulelea yatima ambayo vimenufaika ni kituo cha Jaamia Til Islamiya,Chumbageni Tupie, Coodwill,Mwakidila,Makorora na Makazi ya Wazee wa Mwanzange.

 

Msaada ambao ameutoa ni Sukari Kg 50,Ngano Kg 50,Mafuta ya kula ndoo kubwa,Majani ya Chai Kg 2 ,Tambi Roba 2,Mchele Kg 100 na Maharage kg 100 ambapo vyakula hivyo vitawasaidia katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani.

 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo Waziri Ummy  alisema ameamua kutoka sadaka hiyo ya futari kwa taasisi hizo na vituo vya kulea watoto yatima na wazee ili kuweza kuwaondole ugumu wa mahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

 

“Nimeona nitoe sadaka ya futari kwa Taasisi na vituo vya kulea watoto yatima na Makazi ya Wazee mwezi wa ramadhani ambao ni wa kufanya toba na mimi kama Mbunge wao nimeona nitoe kile alichojaliwa kwao”Alisema

 

Hata hivyo aliwahimiza watu kuendelea kutoa sadaka kwa watu wenye uhitaji ikiwemo kwenye Taasisi zenye uhitaji mkubwa ili kuweza kuwapunguzia makali hususani kwenye kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa ramdani.

 

Awali akizungumza baada ya kupokea msaada huo Katibu wa Idara ya Taaluma wa Taasisi ya Maawal Islamic Mohamed Shabani alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo wa sadaka ya futari ambao amewapatia ambao utawasaidia kwenye kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa mwezi wa ramadhani.

 

Alisema kikubwa wao ni kuhakikisha wanaendelea kumuombea kwa mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwenye kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuweza kutimiza malengo yake

 

“Kwa kweli tunamshukuru Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wetu wa Tanga kwa msaada huu na tutaendelea kukuombea kwa mwezi mungu akuongeze na akufungulie Milango kwenye safari yao”Alisema

 

Naye kwa upande wake -Mwalimu wa Taasisi ya Jaamia na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtupie Saidi Juma  alimshukuru Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga kwa msaada huo wa futari ambao amewapatia huku akieleza kwamba wataendelea kumuombea mwenyezi Mungu amfanyie wepesi.

 

Zoezi hilo la ugawaji wa futari kwa taasisi za dini na vituo vya kulea watoto yatima ikiwemo makazi ya wazee limekuwa likifanyika kila mwaka

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages