Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amependekeza jina la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama Mapinduzi na kushika nafasi ya aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Bashiru Ally.
Hayo yametokea leo Mkoani Dodoma leo Aprili 30, 2021 mara baada Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kushika kijiti cha aliyekuwa Mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

No comments:
Post a Comment