A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 17, 2021

ZANTEL YAZINDUA ‘PASUA ANGA KI ZANTEL 4G’ KUWAELIMISHA WATEJA JUU YA UMUHIMU WA MTANDAO WA 4G

 Caption%2B1

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Zantel, Aneth Muga akicheza mchezo wa Foosball pamoja na Mohammed Waziri mmoja wa wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ uliofanyika katika viwanja vya Kisonge Unguja. Kampeni hiyo imelenga kuwaelimisha wateja juu ya umuhimu wa mtandaowa 4G katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Screenshot%2B2021-03-17%2Bat%2B11.22.26
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Zantel, Aneth Muga pamoja na Issa Chapu wakicheza mchezo wa kikapu (Table tennis) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ uliofanyika katika viwanja vya Kisonge Unguja-Zanzibar. Kampeni hiyo imelenga kuwaelimisha wateja juu ya umuhimu wa mtandaowa 4G katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
ZBC%2B2
Mkuu wa Zantel - Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Zantel ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uchukuzi - Wizara ya Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Mzee Suleiman Mndewa na Zuena Ali, Mjasiriamali mdogo. Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.

Na Mwandishi wetu | Zanzibar | Kampuni ya simu ya Zantel jana Machi 16, 2021 imezindua kampeni yake mpya ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ inayolenga kuwaelimisha wateja juu ya uhumimu wa mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Kisonge mjini Unguja ambapo wananchi wameweza kushiriki na kujionea ni namna gani wanaweza kutumia mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.

Kabla ya uzinduzi huo, Kampuni ya Zantel iliendesha mjadala ulijadili juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G ambao uliruka kupitia televisheni ya ZBC. Mdahalo huo ulihusisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini pamoja na wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa mjadala huo, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Khamis Mussa alisema “Nia yetu ni kunaendelea kuboresha mtandao wetu ili mawasiliano yapatikane Zanzibar yote kwa kasi ya 4G kumuwezesha mtumiaji kuweza kufanya mawasiliano bora na ya haraka. Na sasa tunazindua kampeni ya PASUA ANGA KI ZANTEL 4G mahsusi ili kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa mbalimbali ya mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G.

Katika uzinduzi uliofanyika viwanja vya kisonge, ulihusisha shughuli mbalimbali ikiwamo michezo ya foosball, tebal tennis, pool table huku washindi wakiibuka na vifurushi vya intaneti ya 4G vya wiki pamoja na zawadi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages