
Na Mwandishi wetu | Nairobi | Kenya | Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo Machi 18, 2021 amelihutubia Taifa kupitia vyombo vya Habari vya Nchi hiyo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais Kenyatta Katika hotuba yake fupi amewatangazia rasmi wakenya juu ya msiba huo mzito waliopata watanzania na kueleza namna ambavyo Nchi hizo mbili zilivyokuwa na ushirikiano mzuru wa kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Aidha amechua hatua ya kutoa pole kwa Serikali ya Tanzania na watanzania wote kwa ujumla na kuwataka Watanzania kuwa na moyo wa uvumilivu na kwamba Taifa la Kenya na Serikali yake lipo bega kwa bega na Tanzania katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kutangaza rasmi siku Saba za maombolezo.
No comments:
Post a Comment