A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 19, 2021

ASKOFU MKUU WA KANISA ANGLIKANA TANZANIA DKT, MAIMBO MNDOLWA AZUNGUMZIA KIFO CHA MAGUFULI.

 



Na:Maiko Luoga

“Awali ya yote tutoe Salamu za pole kwa Familia ya Mhe, Hayati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, Ofisi yake, Baraza la Mawaziri, Watumishi, Watanzania, Rais na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Msiba huu mkubwa”

“Msiba huu licha ya kugusa Serikali pia umetugusa sisi Kanisa Anglikana Tanzania umegusa mioyo yetu sote ni Msiba uliotukuta katika kipindi kigumu, katika historia ya Nchi yetu huyu ni Rais wa kwanza kufariki akiwa madarakani”

“Hatuwezi kusema ameacha pengo lakini tuseme ametuachia funzo na somo kubwa kwetu Kanisa na Nchi kwa ujumla, Rais Dkt, John Magufuli kwa wale ambao mtakumbuka alikuwa karibu sana na Viongozi wa Dini tukishauriana kwa karibu”

“Mwaka 2018 nilipoitwa kutumika kama Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania nilionana nae kwa mazungumzo ili kushauriana yale ambayo tunafikiri juu ya Kanisa na Nchi yetu kwa ujumla na katika Mkutano ule mbele ya Waandishi wa Habari nakumbuka nilisema maneno haya Kazi ya Kanisa ni kuomba”

“Tangu wakati ule tuliendelea kumwombea na kumshauri wakati wote tulipokutana na Changamoto na tuliendelea kuwa karibu nae kama ambavyo tulishuhudia akiita Viongozi wote wa Kidini katika Ofisi zake za Ikulu Jijini Dar Es Laam”

“Nyakati zote alipokuwa akifanya mambo makubwa ya Kitaifa alishirikisha Viongozi wa Dini ili tupate kuomba nae na kuombea mambo hayo ili yaweze kwenda vizuri, Mkutano wetu wa mwisho ulikuwa kwenye Uzinduzi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji tuliombea kazi ile na tunashukuru inaendelea vizuri”

“Mhe, Magufuli anapotuacha tunakumbuka kazi alizozifanya enzi za uhai wake pamoja na mchango wake mkubwa Kijamii na Kanisa sio kwa Wakristo pekee bali hata kwa wenzetu Waislamu alikuwa mstari wa mbele kutoa mchango wake wa mawazo na Sadaka”

“Tunajua kazi kubwa inayofanyika huko Dodoma ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa Kiislamu tunakumbuka michango yake aliyokuwa akiitoa alipoingia Misikitini na Makanisani alichangia salamu na sadaka, alikuwa Muumini sahihi Muumini wa wakati na Muumini wa kujitoa”

“Kuondoka kwake ni Mguso mkubwa kwa Kanisa na Taifa, kwa kipindi hiki tunashauri tutazame kazi kubwa aliyokuwa amekabidhiwa na Mungu ambayo aliishika kwa kipindi kifupi sana Miaka hii sita lakini tunaona mchango wake mkubwa usiopimika katika ujenzi wa Taifa”

“Tumeona ujenzi wa miundombinu katika Nchi yetu, tunaona mchango wake mkubwa katika kujenga mahusiano ya Kidini na kuimarisha Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika”

“Rais Magufuli anatuacha tukiwa Taifa moja lenye mshikamano ulio wazi tunaona mchango wake mkubwa katika kuimarika Utalii Nchini pia katika mambo mbalimbali ya maendeleo ambayo hatuwezi kutaja mojamoja hayo yote ni alama alizotuachia”

“Ukitembea katika Barabara zetu unaona jinsi zilivyoboreshwa ukipita Ubungo na maeneo mbalimbali ya Nchi yetu utaona alama za kazi alizotuachia Rais Magufuli”mom

“Katika kipindi hiki yanaweza kusemwa mengi lakini sisi kama Kanisa Tuseme tuendelee kumwombea yeye na Familia, Mungu alimleta kwa wakati na Wakati huo Mungu aliokusudia aitende kazi yake sasa umetimia”

“Changamoto inayobaki kwetu ni kuendeleza pale alipotuachia, Tunamwombea sana Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kazi kubwa iliyopo mbele yake ni kuimarisha haya ambayo ameyaacha Ndg, yetu John Magufuli”

“Tuliombe Kanisa Anglikana Tanzania Baba Maaskofu, Makasisi, Mashemasi, Wainjilisti, Watawa na wengine wote Msiba huu umetokea wakati wa Kwaresma tunapofunga na kuomba kwaajili ya mambo mbalimbali ya huduma katika Kanisa pia tuiombee Nchi yetu”

“Tuiombee Familia ya Hayati Dkt, John Magufuli na kuiombea Ofisi ya Rais, tuwaombee wote wanaoshughulika na maandalizi ya kumpumzisha mpendwa wetu, BWANA NI YEYE ALIYETUPA NA NI YEYE SASA AMETWAA Jina lake lihimidiwe na kubarikiwa kwa Jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU AMEN" Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Dkt, Maimbo Mndolwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages