Rais wa Kosovo Hashim Thaçi amejiuzulu ili kukabiliana na mashtaka dhidi yake yalityotolewa na Mahakama Maalum ya Hague juu ya uhalifu wa kivita wakati wa mzozo dhidi ya vikosi vya Serbia mwishoni mwa miaka ya 1990.
Hashim Thaçi, 52, kiongozi wa zamani wa kisiasa wa kundi la waasi wa waliojitenga la UCK, ameendelea kutawala maisha ya kisiasa ya Kosovo kwa miongo miwili.
"Kama nilivyoahidi, sitakubali kwa mazingira yoyote kwamba nifike mbele ya mahakama kama Rais wa Jamhuri ya Kosovo," Hashim Thaçi amesema katika mkutano na waandishi wa habari.
"Kwa hivyo, kutetea uadilifu wa mamlaka ya rais na Kosovo, pamoja na hadhi ya raia wake, ninajiuzulu kwenye wadhifa wa rais wa Jamhuri ya Kosovo", ameongeza.
Hashim Thaçi ameendelea kusema kuwa hana hatia katika mzozo wa miaka ya 1998-99, akituhumu mahakama ya kimataifa kwa "kuandika historia upya". Watu wengi huko Kosovo wanaona mzozo huu kama "vita vya haki" dhidi ya ukandamizaji wa Serbia.
"Hizi sio nyakati rahisi kwangu na kwa familia yangu, na kwa wale ambao wameniunga mkono na kuniamini katika miongo mitatu iliyopita ya kupigania uhuru, uhuru na ujenzi wa taifa," amebaini Hashim Thaçi.
Mashitaka ya mauaji, visa vya watu kutoweka, mateso yalitolewa mnamo mwezi Juni.
No comments:
Post a Comment