KIPA mkongwe Juma Kaseja amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia nyumbani na ugenini katikati ya mwezi huu.
Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje pamoja na Kaseja wa KMC, pia amewaita 'Tanzania One', Aishi Manula wa Simba SC, Metacha Mnata wa Yanga SC na David Mapigano Kisu wa Azam FC.
No comments:
Post a Comment