A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, September 14, 2020

YANGA YAILAZIMISHA MBEYA CITY 1-0 DIMBA LA MKAPA.


Timu ya Dar es Salaam Yanga African  imeibuka na ushindi kwa kuichapa Mbeya City bao 1-0 Katika Mchezo wa ligi kuu wa msimu wa 2020/21 katika uwanja wa Mkapa dhidi ya Mbeya City Septemba 13,2020.
Kikosi cha Yanga ambacho kina muunganiko wa Wachezaji wapya wengi, kimefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 ikiwa ni goli pekee lililofungwa na Lamine Moro dakika ya 86.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC kuwa na point 4 sawa na Wapinzani wao wa jadi Simba SC ambao nao wameshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja.
Sasa Yanga anaanza safari ya kwenda Bukoba kucheza dhidi ya Kagera Sugar September 19 na baadae kurejea Morogoro September 27 2020 kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Mbeya City wao kwa sasa hawana point baada ya kupoteza mechi 2 zote za mwanzo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages